WANANCHI MUSOMA VIJIJINI WAJITOLEA UJENZI WA ZAHANATI.
![]() |
Wananchi wakiwa pamoja na Mbunge wa Jimbo hilo mara baada ya kikao cha pamoja kujadili maendeleo |
Jimbo la Musoma Vijijini lenye Vijiji 68 na
Kata 21 limeanza utekelezaji wa ujenzi wa zahanati kila kijiji ikiwa ni utekelezaji wa
Ilani ya chama cha mapinduzi.
Jimbo hilo la musoma vijijini lina Zahanati
29 zinazotumiwa kwa matibabu na Zahanati mpya 9 zinajengwa kwa kutumia michango
na nguvu za wananchi wakishirikiana na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo (Prof Sospeter
Muhongo) .
Mbunge wa Jimbo alifanya zaiara jimboni humo
akishirikiana na ameshirikiana na Madiwani pamoja na Wakazi wa Kijiji cha Kurwaki
nakufanikiwa kuchangia mifuko ya saruji
zaidi ya 350 kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Kurwaki.
Kijiji cha Kigera Etuma kimeamua kujenga
zahanati kijiji ni baada ya kukosa kituo cha afya na Zahani kwa muda mrefu
jambo ambalo limepelekea wananchi wa kijiji hicho kutembea umbali takribani Km
5 hadi saba kutafuta huduma katika kata jirani.
“Ambapo sasa Jengo la Matibabu (OPD) limekamilika kwa
Asilimia 80 na nyumba ya Mganga na Muuguzi (two in one) inajengwa kwa
kasi kubwa sana. Lengo ni kukamilisha ujenzi wa majengo hayo 2 ifikapo Desemba
2018” alisema Diwani wa kata ya Nyakatende.
Aidha Wachangiaji
wa ujenzi wa Kijiji cha Kigera Etuma ni Wafadhili na Wakazi wa Kijiji hicho Mbunge, Madiwani na Wananchi wamechangia
misumari, nondo na mifuko 150 ya saruji.