MAASKOFU 34 KATOLIKI WAOMBA KUJIUZULU.

Maaskofu hao wanatuhumiwa kwa kuzuia uchunguzi wa kashfa ya ngono inayomuhusu Kasisi mmoja anayetuhumiwa kwa kumlawiti mtoto mdogo wa kiume.
Kashfa hiyo inamhusu Askofu Juan Barros ambaye anatuhumiwa kutumia wadhifa wake ndani ya Kanisa Katoliki kujaribu kuzuia uchunguzi dhidi ya tuhuma za udhalilishaji kingono zinazomkabili Kasisi Fernando Karadima.