VIDEO MAKALINEWS.RC MALIMA WATAKAO KOSA KITAMBULISHO CHA UTAIFA MARA KUKIONA.

MKOA wa Mara umetajwa kuwa mkoa wa kwanza nchini kumaliza zoezi la usajili na utambuzi wa wananchi wake katika kipindi cha muda wa siku 90 sawa na malengo iliyojiwekea.
Hatua hiyo imekamilika kwa kusajili wa jumla ya watu 718,647 kati ya 763,142 waliotakiwa kusajiliwa kuzingatia takwimu za idadi ya watu wenye umri wa miaka 18 na kuendelea hivyo kufikia asilimia 94 ya lengo la mkoa huo.
Mkuu wa mkoa huo Adam Malima alisema hayo Jana alipokuwa akitoa taarifa kwa waandishi wa habari mkoani hapa, kuhusu mwenendo wa usajili wa wananchi wa awamu ya kwanza kwa ajili ya kupata vitambulisho vya Taifa.
"Kupitia zoezi hili tumefanikiwa kusajili jumla ya wageni wakazi 224 wanaoishi kihalali Mkoani Mara, ikumbukwe Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA) inatoa vitambulisho vya aina tatu Raia, Mgeni na Mkimbizi.kwa hiyo kama bado kuna wagen ambao hawajasajiliwa nawashauri nao wajitokeze wakasajiliwe"alisema Malima.
Alisema kwa sasa uongozi wa mkoa kwa kushirikiana na kamati za ulinzi na usalama za wilaya, vijiji na mitaa wanaendelea taratibu za kuchakata taarifa za waombaji wote ili kuhakikisha kila mwananchi anapita Kwenye Chujio la uraia kisha uzalishaji vitambulisho unaendelea kutekelezwa na ifikapo mwezi mei mwaka huu kuanza rasmi ugawaji wa vitambulisho hivyo kwa wananchi.
Kwa upande wake Afisa usajili wa Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa( NIDA) mkoani hapa Ohana Gerald alisema wilaya za Musoma na Bunda ni wilaya zilizofanya vizuri zaidi katika zoezi hilo ambapo wamefanikiwa Kusajili kwa asilimia 112 ya malengo waliokuwa wamejiwekea.
"Tunakusudia kuweka awamu ya pili na ya mwisho kuanzia mwezi mei hadi juni mwaka huu kwa wale wote ambao hawakubahatika kusajiliwa wakiwemo wale wabishi ambao hawafanyi jambo bila kusukumwa kujitokeza kwa wingi"alisema Ohana.
Kaimu Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano(NIDA) Rose Joseph ametoa wito kwa wakuu wa Mikoa mingine wanaoendelea na zoezi hilo kutumia mfumo ambao umetumiwa na uongozi wa mkoa wa Mara ili kurahisisha na kuharakisha zoezi hilo linaloendelea kutekelezwa nchini note.
"Tumefarijika kuona kwamba zoezi ambalo tulikuwa tumekusudia lifanyike mkoa wa Mara kwa muda mfupi limekamilika, sisi kama mamlaka Tupo tayari kutoa ushirikiano kwa viongozi wakuu wa mikoa mingine kwa kutoa vifaa vya kutosha, pia tumejifunza hapa Mara kuwa viongozi wa mkoa waliweka kipaumbele zoezi hili la usajili" alisema Rose.
Mwisho.