KAULI YA MANDAWA KABLA NA BAADA YA KUITWA TAIFA STARS.



Mshambuliaji Mtanzania anayeichezea klabu ya BDF XI inayoshiriki Ligi Kuu Botswana, Rashid Mandawa, amezungumza kwa mara ya kwanza baada ya kuitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars.

Mandawa ambaye ameitwa kwenye kikosi hicho baada ya kupigiwa kelele na mashabiki pamoja na baadhi ya wadau wa soka, amesema anashukuru na anaheshimu maamuzi ya Kocha Salum Mayanga kumuongeza kwenye timu.

Aidha, Kwa mujibu wa Sports HQ ya EFM Radio, Mandawa ameeleza kuwa kabla hajaitwa Taifa Stars alikuwa anatumia muda wake kusali ili apate nafasi ya kuchaguliwa kwenye kikosi hicho.

Ikumbukwe baada ya kikosi cha kwanza kutangazwa na Kocha Salum Mayanga, Mandawa hakuwepo na baadaye ikazua maswali iweje aachwe ilihali anafanya vizuri kwenye ligi ya Bostwana.

Tayari mchezaji huyo alishasafiri kuelekea Algiers ambapo Taifa Stars itacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Algeria, Machi 22 2018.
Powered by Blogger.