SUGU, MASONGA MIEZI 5 JELA KWA KOSA LA KUTUMIA LUGHA YA FEDHEHA DHIDI YA MHE. RAIS.



Mbeya. Mbunge wa Mbeya mjini (Chadema) Mhe. Joseph Mbilinyi ‘Sugu’na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga wamehukumiwa kifungo cha miezi mitano jela baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais Magufuli.
Akisoma hukumu hiyo asubuhi ya leo Jumatatu Februari 26, 2018, Hakimu Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya, Michael Mteite, amesema kuwa Sugu na Masonga walitenda kosa hilo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Desemba 30, 2017 eneo la Uwanja wa Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya.

“Mhe. Rais hawezi kupendwa na watu kwa kumshoot risasi Lissu, kumtupa jela miezi minne Lema, kumteka Ben Saanane, kumteka Roma, na kumzuia Sugu asiongee”, ni baadhi ya kauli zinazosemekana kutolewa na Mhe. Sugu.

Madai ambayo ni kumkosea heshima Amri Jeshi Mkuu wa nchi kwa kumhusisha na vitendo ambavyo amekuwa akivipinga na kulitaka jeshi la polisi kuchua hatua dhidi ya wote wanaohusika.

Katika hatua nyingine, wakili wa washtakiwa aitwaye Boniphace Mwambusi amesema wanakwenda kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo, huku mahakama ikiwapa muda wa siku ya leo pekee kuwa tayari wamekwisha wasilisha rufaa yao.
Powered by Blogger.