MCHUNGAJI ELINAFIKA MOLLELI ;AITAKA JAMII KUMUOGOPA MUNGU NAKUACHA UKATILI MKOANI MARA .

Mch. Elinafika Molleli.
sehemu ya wanafunzi waliohudhuria kongamano hilo Mchungaji Elinafika Moleli wa kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania Usharika wa Musoma mkoani Mara , na ambaye ni mratibu wa dawati la utetezi na maswala ya ukatili wa kijinsia ameitaka jamii kuacha kuendeleza mila ptofu zikiwemo za ukeketaji kwa mtoto wa kike kwani huko ni kukosoa uumbaji wa Mungu , na kuwakosea wanawake wote na watoto wa kike kwa ujumla .
Aliyasema hayo katika kongamano la wanafunzi wa shule za msingi na sekondari la kupinga ukatili na unyanyasaji lililofanyika katika viwanja vya shule ya sekondari Suba, Mchungaji Moleli ameitaka jamii kumuoga Mungu kwa kutoingilia ukosoaji wa kimaumbile ambao umekuwa ukifanywa kwa kisingizio cha kuendeleza mila katika jamii , kitu ambacho kimekuwa kikiwaacha wasichana na maumivu makubwa na kusababisha kuvuja damu nyingi wakati wa kujifungua .
Alisema imefika wakati ambao jamii lazima ielewe kwa kina na ipate elimu ya kutosha ya madhara ya ukatili huo wa kijinsia na ukeketaji ili iweze kuacha kufumbia macho vitendo kama hivyo kwa kukemea kuanzia ngazi za familia.
Aidha amelipongeza shirika la moyo safi wa Maria Afrika , Baraki Sisters Farm waandaaji wa kongamano hilo la wanafunzi la kupinga ukatili na unyanyasaji kwa shule za msingi na sekondari na kuwataka kuzidi kutoa elimu zaidi ili kuhakikisha jamii inaondokana na ukatili ikiwemo utamaduni wa kukeketa .
kongamano hilo la kupinga ukatili wa kijinsia na unyanyasaji , liliandaliwa na Shirika la moyo safi wa Maria Afrika, Baraki Sisters Farm , kwa ufadhili wa the foundation for civil Society, ambapo limehusisha shule za sekondari na msingi zilizopo katika kata 13 za Wilaya ya Rorya, ambazo mradi huo unatekelezwa.