MWANAMKE ACHOMWA MOTO KISA KUKU..



 Na MAKALIBLOG.MARA
Mkazi wa mtaa wa Bugosi katika halmashauri ya mji wa Tarime, mkoani Mara, Anna Jeremia (45), amenusurika kifo baada ya kumwagiwa petroli na wanamtaa wenzake Kisha kuwasha Moto kwa kiberiti akidaiwa kuiba kuku.

Akizungumza akiwa amelazwa katika wodi namba sita kitandani na 17, katika Hospitali ya mji wa Tarime huku akiongea kwa maskitiko, Jeremia aamesema kadhia hiyo ilimkutaka Novemba 4 majirq ya Asubuhi baada ya manyoya ya kuku karibu na Nyumba Yale.

"Nilishangaa wanakuja kwangu nanilazimisha nikubali kuba kuku, wakaagiza Mafuta ya peteroli wakanimwagia na kuwasha kiberiti nikaanza kukimbia nasema Mungu wangu akanisikia Moto ukazima, kwa Sasa kifua ndicho kinauma pamoja na macho,"alisema mama huyo.

Alizitaka mamlaka za kisheria kusimamia ukweli dhidi ya shauri lake.

"Kuna vijana wengi karibu na jnapoishi ambao nap walikamatwa kwa nini Mimi ndiye nichomwe wakati nao walikamatwa, sheria ifuate mkondo wake ili kupata uhakika, kazi yangu Mimi ni kuuza mifagio,"alisema Jeremia.

Binti yake akimuuguza, Maria Jeremia alisema kuwa kitendo alichofanyiwa mama yake na wanamtaa ni Cha kufedhehesha na hakikustahili kwa kuwa si mwizi na kupatikana kwa manyoya karibu na Nyumba yake si kigezo Cha kumtuhumu kuwa ni mwizi

"Naomba serikali iwakate waliohudika kufanya ukatili huu kwani wamemwonea mama,"alisema Jeremia.

Naye kijana wake mama huyo Musa Mtete alisema waliifanya kitendo hicho ni viongozi wa mtaa ambao ndio ulitakiwa kumtetea.

"Wanajua kuwa Hana mtu wa kumwonea huruma kwa kuwa anakunywa pombe, kitendo ambacho si Cha kiungwa kwa viongozi kuongoza kitendo hiki Cha ukatili,"alisema Mtete.

Akizungumzia Hali ya Maendeleo ya afya yake Mganga mfawidhi wa Hospitali hiyo Lipolight Tarimo alisema walimpokea siku ya jumamosi baada ya kufikisha na gari la polisi na alipochnguzwa ilibainika amechomwa na kimimimika Cha Moto kichwani, usoni na kifuani lakini hali yake inaenda vizuri.

"Hali ya mgonjwa kwa kweli ni nzuri kwa sasa baada ya madaktari na manesi wetu kufanya kazi ya kumhudumia tangu tumpokee siku ya jumamosi saa tano Asubuhi, "alisema Tarimo.

Wiki iliyopita mwanaume Mmoja katika maspaaa ya Musoma amefahamika kwa jina la Aloyce Raymond alimwagia maji maji ya Moto na mke wake kwa sababu ambazo zilidaiwa hazina mashiko kwa kmushindwa kutoa matumiz alipokuwa akiondoka nyumbani kwake na baada ya kufanyiwa hivyo Ngozi ya mgongoni.mikononi na miguu ikabanduka.
Powered by Blogger.