DKT.ANNA MAKALA...WANAOHIFADHI WAHAMIAJI HARAMU KUKIONA
MAKALIBLOG.MARA
Serikali imesema kuwa itawachukua hatua Kali watu wanaojihusisha na uifadhi wa wahamiaji haramu kwa kuwapatia hifadhi pamoja na kuwasafirisha badala ya kutoa taarifa kwa vyombo husika.
kauli hiyo imetolewa Jana na Kamishna Jenerali wa idara ya uhamiaji nchini, Dk. Anna Makakala alisema kuwa wananchi hususani waishio mipakani wamekuwa wakiwapokea na kuwahifdahi wahamiaji haramu katika miji Yao jambo ambalo alisema kuwa ni kinyume cha sheria ya uhamiaji ya mwaka 2016.
Alisema kuwa wananchi waishio mipakani wanapaswa kushirikiana na serikali katika suala zima la
ulinzi na usalama wa nchi kwa maelezo kuwa kuishi na wahamiaji haramu nchinini kunahatarisha wa nchi kwa kiasi kikubwa.
Dk. Makakala alisema kuwa Kila raia wa Tanzania analo jukumu la ulinzi wa nchi na kwamba wanapaswa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama katika kuibua na kutoa taarifa juu ya uwepo wa wahamiaji haramu pamoja na viashiria vya uvunjifu wa amani katika makazi yao.
" nawaomba wananchi wasitumie muingiliano uliopo katika mipaka yetu kukwepa kutimiza wajibu wao wa ulinzi katika mipaka hii na badala yake watoe taarifa kwa vyombo vyaulinzi na usalama juu ya wahamiaji haramu wanaingia nchini ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi Yao kabla ya kuhatarisha usalama wanchi yetu" alisisema makakala.
Aliongeza kuwa mbali na kuwahifdahi na kuwaficha wahamiaji katika maeneo yao pia kumekuwepo na tabia ya baadhi wamiliki wa vyombo vya usafiri wakiwemo waendesha piki piki maarufu kama boda boda kuwaingiza na kuwasafirisha wahamiaji haramu nchini kinyume cha sheria ambapo alitolea mfano mji wa Sirari wilayani Tarime ambapo bodaboda wamekuwa wakiwaingiza wahamiaji haramu nchini kwa kutumia njia zisizo rasmi.
Kufuatia kuwepo kwa hali hiyo Dk. Makakala amewaagiza wamiliki wa vyombo vya usafiri kuacha Mara moja tabia hiyo na kwamba watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo mbali na kufikishwa mahakamani serikali pia itataifisha vyombo vyao vya usafiri.
Mwisho