WANANCHI WA SEGESE WAWAJIA JUU WATU WALIOJENGA NYUMBA ZA MAKAZI NDANI YA KIWANJA CHA ZAHANATI.

Wakazi wa kijiji cha Senta ya Mashariki Kata ya Segese Halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga wameomba watu wote waliovamia eneo la Zahanati ya kata hiyo kuondolewa ili kupisha ujenzi wa uzio wa Zahanati hiyo unaoendelea kujenga.

Wakizungumza na Kijukuu Blog kwa nyakati Tofauti wamesema kumekuwepo na Urasimu wa kuwaondo watu waliovamia eneo hilo kwani wapo ambao nyumba zao zipo katika eneo la Zahanati lakini nyumba zao hazikutakia kubomolewa.
Wamesema mipaka ya Zahanati hiyo inafahamika lakini hivi sasa inapindishwa jambo ambalo linasababisha kuwaonea baadhi wananchi ambao wanaishi jirani na eneo hilo.

MARTINE KUSEG’WA ni miongoni mwa wakazi wa kijiji cha Senta Mashariki, ambaye amedai kuonewa na baadhi ya viongozi wa kijiji hicho kwani wameweka uzio wa Zahanati hiyo hadi kwenye Nyumba yake.

Mwenyekiti wa kijiji hicho PIUS EDWARD IGUHA amesema eneo hilo linamgogoro wa Muda mrefu, na tayari ofisi yake ilishapokea barua kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI ikieleza kuwaondoa watu wote waliovamia maeneo ya wazi ukiwemo hilo la Zahanati.

Eneo hilo lilitengwa na kijiji hicho mwaka 1985 likiwa na ekari 2, lakini hadi sasa limebaki nusu ekari.

MOJA YA NYUMBA AMBAYO INADAIWA KUJENGWA NDANI YA KIWANJA CHA ZAHANATI YA SEGESE.
CHOO CHA ZAHANATI KIKIWA KIMEPAKA NA NYUMBA YA MKAZI MMOJA AMBAYE NAYE AMEJENGA NDANI YA KIWANJA CHA ZAHANATI.
Powered by Blogger.