WANANCHI BARIADI WAMPONGEZA RAIS, DC ANENA!!: PICHA ZA MATUKIO YOTE ANGALIA.



Mabango yenye jumbe mbalimbali.


katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Bariad Festo Kiswaga katika kongamano la wanachi
kupongeza kazi inayofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh
John Magufuli

wananchi wa Simiyu wanatarajia kunufaika na mradi mkubwa
wa maji ya Ziwa Victoria utakaogharimu kiasi
cha Shilingi Bilioni 340.2 kukamilika kwake na kuwaondolea adha
kubwa waliyokuwa wakiipata kwa miaka mingi toka kuanzishwa kwa Mkoa huo.

hayo yalibainishwa jana Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Festo Kiswaga wakati
wa kongamano kubwa la kumpongeza Rais John Magufuli katika
utendaji wake wa kazi, lililofanyika katika viwanja vya midimi mjini Bariadi.

kuwa wananchi wa Wilaya yake ya Bariadi na Mkoa mzima wataanufaika
na mradi huo mkubwa wa maji ya ziwa victiria ambao ukikamilika
utawaondolea kero ya kutumia mda mwingi kusaka maji.

Kiswaga alieleza kuwa katika kongamano lililofanyika jana la
kumuombea na kumpongeza Rais Magufuli ,wananchi hao wamemshukuru
sana Rais Magufuli kwa kuwapatia kiasi hicho kikubwa cha fedha ambacho
hawakuwahi kutarajia kama wanaweza kufanikiwa kutatua tatizo la maji ambalo
limetanda ndani ya Mkoa wa Simiyu.

Aidha Kiswaga alisema kuwa mbali na kutolewa kiasi hicho cha fedha kutoka kwa Rais
Magufuli pia wameongezewa kiasi cha shilingi Bilioni 86.8
kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Baraidi Maswa ambayo inayojengwa kwa kiwango
cha lami.


Kwa upande wa wananchi wa Wilaya ya Bariadi wamemshukuru Rais Magufuli kwa kutoa kiasi hicho
kikubwa cha pesa ambacho kitawasaidia kupata huduma ya maji safi na
salama pamoja na miundombinu mizuri ya barabara ambayo imekuwa kero
kubwa kwao tangu uhuru.

Sambamba na hilo viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini Mkoani
Simiyu wamefurahishwa na miradi mikubwa ya afya,barabara,maji na
elimu inatekelezwa kupitia fedha zilizotolewa na rais
Magufuli.

mchungaki wa kanisa la AICT Amos Ndaki alisema kuwa watanzania wote wanapaswa kuombea amani ya
nchi yao na kuungana kwa pamoja katika kufanya kazi kwa bidiii ili
kumuunga mkono Rais Magufuli.



Burudani.
Powered by Blogger.