Ronaldo amfunika Pele, matokeo yote kufuzu kombe la dunia


Mshambuliaji wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo amefanikiwa kumzidi idadi ya mabao mfalme wa soka Edson Arantes do Nascimento ‘PELE’ baada ya kufunga ‘hat trick’ katika mchezo dhidi ya Faroe Islands hapo jana.

Akifunga hat trick yake ya 48 katika maisha yake ya soka iliiwezesha Ureno kutwaa alama tatu muhimu katika mechi hiyo ya mbio za kuwania kushiriki kombe la Dunia 2018 litakalofanyika nchini Urusi.



Ronaldo ameweza kumfunika nguli huyo wa soka kwa kufikisha idadi ya mabao 78 ikiwa ni bao moja zaidi yake ambaye amepachika mabao 77 katika mechi za kimataifa ikijumuishwa na magoli katika michezo ya kirafiki.

Ronaldo sasa anaifukuzia rekodi ya mabao ya muda wote barani Ulaya inayoshikiliwa na Ali Daei aliyepachika mabao 109.



Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chin
Powered by Blogger.