MKELEKETWA WA SOKA ATOA MSAADA WA JEZI KWA BIASHARA UNITED MARA;



kulia ni Ayoub konshuma akikabidhi jezi kwaniaba ya mdau ni katika uwanja wa posta mjini musoma


Baadhi ya wachezaji wa biashara unite mara





Na makaliblog, MARA
Uongozi wa timu ya Biashara United inayojiandaa ushiriki wa ligi daraja la kwanza Tanzania Bara umepokea msaada wa jezi pea mbili kutoka kwa mdau wa soka, hatua ambayo imeelezwa itasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri katika ligi hiyo.

Mwenyekiti wa kamati ya fedha na mipango katika klabu hiyo marwa mathayo alisema kuwa msaada huo utawasaidia kwa kiasi kikubwakuleta matokeo mazuri katika klabu ya Biashara United Mara katika ligi hiyo.

“Kwaniaba ya uongozi wa timu ya Biashara united mara tunashukuu sana kwa msaada huu na tunaomba wadau wasoka popote walipowazidi kujitokeza kuhakikisha timu hii inafanya vizuri kwani hii ni timu yetu sote “alisema mwenyekiti huyo.

Akikabidhi msaada huo kwa niaba ya mdau huyo wa soka Ayoub konshuma alisema mssada huo umeonyesha nia njema ya wana mara katika kuhakikisha timu hiyo inapanda ligi kuu.

katika hatua nyingine meneja wa timu hiyo Aman Josiah alisema kikosi cha biashara united mara kiko katika hali nzuri na wachezaji wapo katika morali kubwa ya ushiriki wa ligi daraja la kwanza itayoanza hivi karibuni.

“tunashukuru kikoso kipo vizur naadhani tutarajie matokeo chanya ila tunachoomba ni wadau waendelee kutupa sapot kwani bado tunahitaji sana msaada” alisema Aman.

Kwa upande wawachezaji wa timu hiyo wameomba kuungwa mkono na wadau mkoani hapa hatua ambayo wameahidi kufanya vizuri katika ligi daraja la kwanza Tanzania Bara.

Timu ya Biashara united mara inashiriki ligi daraja la kwanza Tanzania Bara baada ya kuchukua nafasi ya timu ya Polis Mara.
Powered by Blogger.