BIASHARA UNITED MARA YAANZA VYEMA LIGI DARAJA LA KWANZA, WAMPIGA TOTO “1” BILA .



sehemu ya mashabiki wakifatilia mechi ya Biashara na Toto afican katika uwanja wa karume mjini Musoma.

Na Mkaliblog; MARA
Timu ya Biashara United Mara yaanza imeanza vizuri michuano ya ligi dara la kwanza baada ya kuipiga Toto African wanakisha mapanda kutoka mwanza kwa bao 1 Kwa bila mechi ambayo imepigwa kunako katika uwanja wa karume mjini musoma mkoani mara.

Mechi hiyo ilikuwa ya ufunguzi wa ligi hiyo ambapo ili wachukua dakika 15 Biashara united mara kupitia kwa mchezaji wake mpapi kuifungia bao hilo la uongozi mpaka dakika 45 za kipindi chakwanza Biashara United mara walikuwa wakiongoza kwa Bao moja kwa bila.

Kipindi cha pili kilianza kwa timu kushambuliana lakini mpaka kipyenga cha mwisho cha mwamuzi Saad Juma kutoka kigoma Biashara United Mara 1 na Toto African 0.

Baada ya mechi hiyo Makaliblog ilizungumza na msemaji wa timu ya Toto African Gasibeth Jaffety yeye alisema hakulidhishwa na maamuzi ya mchezo huo kwani bao lilofungwa lilikuwa lakuotea hivyo hawaoni hofu yoyote kwa Biashara United ambapo wameahidi kufanya vyema katika mechi ya marudiano .

“ Sijaridhika na maamuzi ya mechi yaleo lakini niwaondoe shaka tu washabiki na wapenzi wa timu ya Toto tutafanya vyema katika mechi ya marudiano Biashara United wanapafahamu vyema pale kirumba”alisema msemaji huyo wa timu ya Toto.

Lakini Makalinewz ilizungumza na mwalimu wa timu ya Biashara United mara Amani Josiah alisema ameyapokea vyema matokeo kwani wamecheza na timu kubwa ambayo ilikuwa ikishiriki ligi kuu na hivyo bado wana mlima mrefu wa kupanda.

Amani amewahidi wana mara kuendelea kuiunga mkono timu yao kwani ushirikiano ndio kitu mhimu kinachotakiwa katika kipindi hiki.

“Tuendelee kushikamana kwani bado tunayo safari ndefu katika ligi hiii ndio kwanza tumeanza lakini naahidi nitawasihi vijana wanagu kupambana nakuiletea heshima mara”.alisema amani.


                                 Tupe MAONI YAKO HAPO CHINI MATUSI (HAPANA)


Powered by Blogger.