AFARIKI DUNIA KWA KUNYWA DAWA ZA MITISHAMBA MARA;



Makaliblog; Mara
Mtu mmoja amefariki dunia kwa kunywa dawa za Mitishamba zinazotembezwa mtaani hivyo kupelekea madhara makubwa mwilini mwake kwani alikuwa akisumbuliwa na tatizo la kufunga kukojoa,ambapo marehemu amefahamika kwa jina la okech kabala mkazi wa Nyamirende huko Wilayani rorya mkoani mara.

Tukio hilo limetokea katika kijiji cha Nyamirende kata ya kinyenche, wilayani Rorya mkoani mara Bwana mmoja ambae alifariki dunia baada ya kutumia zawa hizo na alipokimbizwa hospitali  ndipo alipopoteza maisha.

maneno ya hapa na pale yakaifanya blog hii kufatiria kwa undani kwani japo ndugu wanakataa kukubaliana na kwamba marehemu hajafa kwa kunywa dawa hizo bali niugonjwa uliokuwa unamsumbua muda mrefu.

Akizungumza  kwanjia ya simu na makaliblog mmoja wa ndugu wa marehemu samweli kabale alisema nduguye huyo amekuwa na tatizo la ugongwa wa kufunga kukojoa nahicho ndio chanzo cha kifo chake japo na dawa hizo alizitumia, lakini hazikuwa na madhaa yoyote kwake alisistiza ugonjwa wake ndio ulisababisha kifo hicho.

“Nikweli ndugu yangu alikuwa na ugonjwa wakufunga kukojoa nahilo ndio tatizo kubwa ambalo naweza sema limesababisha kifo sivile inavodaiwa alikunywa dawa za masai hapana japo alikunywa lakini hazikuwa na madhara yoyote kwake,alisema” samweli

Na Baada ya taarifa hizo zilithibitishwa na mwenyekiti wa serikali ya kijiji ambapo alisema kuwa taarifa alizopata kutoka kwa raia wema marehemu alikuwa na ugonjwa wa tatzo la kufunga kukojoa japo maneno mengine ambayo yalikuwa yakisikika nikwamba marehemu alijaribu kutumia dawa za masai ambazo ndio chanzo cha kifo chake hivyo alitumia nafasi hiyo kuwataka wananchi kuacha kutumia dawa hovyo bali wazingatie vipimo.
Powered by Blogger.