AUAWA KWA KUCHOMWA KISU BAADA YA KUMTUHUMU MPENZI WAKE KACHEPUKA;



Na makaliblog;
MSICHANA mwenye umri wa miaka 25, Janet Mwenda anashikiliwa na Polisi mkoani Mara kwa tuhuma ya kumuua kwa kisu mpenzi wake, Mgini Aaron (37).

Mauaji hayo yalitokea juzi saa 11 jioni katika Kitongoji cha Kitaramanka Kijiji cha Magunga Kata ya Mirwa wilayani Butiama, ambako mtuhumiwa huyo alimchoma kisu hicho katika titi la kushoto na kusababisha kifo cha mpenzi wake huyo.

Akithibitisha mauaji hayo, Kamanda wa Polisi wa Mara, Jafari Mohamed alisema chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa mapenzi, baada ya Janet kufika nyumbani akitoka matembezini na kuingia bafuni kuoga na ndipo mpenzi wake alipomtuhumu kwa kumsaliti huko alikotoka.


Kamanda Mohamed alisema Aaron alipoona mpenzi wake akioga, aliona si hali ya kawaida na ndipo alipoanza kumpiga kwa kumtuhumu kusaliti na ndipo mtuhumiwa alipochukua kisu na kumchoma na kusababisha kifo chake.


Akizungumza na MAKALIBLOG kwa njia ya simu Afisa mtendaji wa mirwa Bi.neema Philipo Alisema pamoja naelimu kubwa ambayo wanaitoa katika maeneo hayo bado matukio hayo yamekuwa yakijitopkeza kutokana na eneo hilo kuna wachimbaji wadogo wadogo lakini bado jitihada nikubwa ilikuweza kuyadhibiti matukio kama hayo kujitokeza.

''mpaka sasa maneno mengi yanazungumzwa kutokana na tukio hilo huku ukweli ukibaki nimajibizano2 yaliyotokea baaina ya hao wapenzi ambao walikutana siku hiyo.Alisema neema''


                                               HABARI NA MATUKIO TUPIGIE NA- 0754295996

                                               TUPE MAONI YAKO( MATUSI HAPANA)
Powered by Blogger.