MAKALIBLOG; VIDEO NA PICHA KATIKA MATUKIO TOFAUTI TOFAUTI YA WANAHABARI WALIVYOTEMBELEA ENEO LA BUHEMBA KUJIONEA KAZI INAYOFANYWA NA STAMICO.TIZAMA
Kaimu mkurugenzi wa STAMICO akitoa taarifa mbele ya wandishi wa habari ya utafiti katika eneo la buhemba. |
alievalia miwani ni Kaimu mkurugenzi wa stamico Mr Alex Rutangwelela kushoto kwake ni mwandishi wa kiyuo cha Azam media wakitembelea maeneo ya wanayoayafanyia utafiti.picha na makaliblog. |
wakiaandaa mitambo kwa ajiri ya kazi |
kaimu mkurugenzi wa stamico Mr Alex Rutangwelela akiwaonyesha wanahabari maeneo ambayo wanachoronga katika eneo hilo la Buhemba. |
wanahabari wakiwa kazini |
mwenye kofia nyekundu ni mmiliki wa makaliblog akiangalia kwa umakini mashine zinavyofanya kazi.
Afisa uhusiano wa (STAMICO) BW. Issa mtuwa akijadili jambo na mwandishi wa gazeti la mtanzani shomari binda alievalia kofia nyekundu..
Na MAKALIBLOG;
Kuwepo kwa matukio ya wachimbaji wadogo kupoteza maisha maeneo ya migodi inawezekana mwarobaini wake umepatikana na baada ya Sirika la madini la Taifa (STAMICO) kwa kushirikiana na wakala ya Jiolojia Tanzania (GST) kupitia mradi wa Usimamizi Ensdelevu wa Rasilimali za Madini inafanya utafiti wa kijiosayansi unaohusisha uchorongaji wa miamba na ukadiriaji wa mashapo ya madini katika maeneo yanayaotarajiwa kuanzishwa vituo saba nchini.
Mradi huo umelenga kuwasaidia wachimbaji wadogo wa madini Nchini ilikufahamu na kupata taarifa za kitaalam za kiolojia katika maeneo waliyopo ikiwemo ukadiriaji wa mashapo.
Pia mardi umelenga kuwatoa wachimbaji wadogo katika uxhimbaji duni kwenda katika uchimbaji wa kati unaotumia teknoloja bora za uchimbaji na uchejuaji ilikuhifadhi mazingira vyema.
Mradi unafadhiliwa na Beki ya Dunia Kupitia Wizara ya Nishati na madini (MEM) na utagharimu kiasi cha USD3.7M sawa na TZS Bilioni 8.2 katika awamu ya kwanza.
Kupitia mradi huu,wachimbaji wadogo watapewa mafunzo na watahamasishwa kutumia teknolojia ya kisasa katika uchimbaji ili waweze kuifanya miradi yao kuwa endelevu na kuwawezesha kukua zaidi.
Utekelezaji wa mradi huu ni hatua muhimu sana kutokanana na faida zitakazo patikana,sio tuu kwa wachimbaji wadogo wa madini bali kwa serikali ambapo kukamilisha kwa vituo hivyo vya mfano kutawawezesha wachimbaji kuacha uchimbaji wa kubahatisha na badala yake watakuwa wanachimba kwa uhakika wa uwepo wa madin.
Kwa upande waserikali kuwpo kwa vituo hivyo vya mfano kama sehemu au chanzo cha serikali kupata tozo kupitia wachimbaji wadogo kwani watakuwa wametambuliwa na kuwekwa katika mpango maalum.
Kazi ya uchorongaji zinazotekelezwa katika maeneo yote ya mradi ,zinafanywa kwa kutumia mitambo ya kisasa ya uchorongaji ya shirika la madini la Taifa( STAMICO) ambayo ina uwezo wa kufanya kazi hizo kwa urahisi na ubora a hali ya juu,Tofauti na awali ambapo mitambo ilikuwa inakodiwa kutoka kwenye makampuni mengine binafsi.
Baaada ya utekelezaji katika maeneo ya BUHEMBA,na MPANDA kukamilika eneo litakalofuata ni Tanga ENEO LA kyerwa ambapo limefanyiwa utafiti wa kijiolojia na halitafanyiwa uchorongaji kutokanan na aina ya mamba na madini (Bati)iliyopo eneo hilo kutohitaji uchorongaji miamba.
TANGA ZA MAKALIBLOG.
TUPE MAONI YAKO MATUSI HAPANA
0754295996 AU mussaj970@gmail.com