WATANZANIA KUNUFAIKA NA GoSol; UNAWEZA KUANGALIA PICHA NA MATUKIO YOTE KATIKA SEMINA HIYO;


Heikki lindfors Field Operation Akionesha mmoja ya mtambo ambao unaweza kuendeshwa na mionzi ya jua ilijiko hilo liweze kufanya kazi.
wandishi wa habari wakipata semina kuhusiana na jiko hilo 




Heikki lindfors Field Operation akitoa mafunzo kwa wandishi.

kaimu mkurugenzi wa bodi ya Global Resource Alliannce  kulia kwake ni Heikki wakijadili na wandishi mara baada ya mafunzo.

jiko linatumia mionzi ya jua kufanya shughuli zake.


Heikki akionesha jiko linavyofanya kazi.

kushoto ni jiko nakulia ni solar ambae imetengenezwa na vioo vya kawaida.

 kushoto ni jiko nakulia ni solar ambae imetengenezwa na vioo vya kawaida.

Kaimu mkurugenzi wa Global Resource Alliance Tanzania Madaraka Nyerere akizungumza na wandishi wa habari.

Anaitwa Benedeta Monika Macha akiwaeleza wanahabari jinsi alivonufaika na GoSol        

Shirika la finland wartsila linijulikanalo kama GoSol  wameadaa mashine inayotumia mionzi ya jua kwa lengo la kuondokana na uharibifu wa mazingira ikiwemo ukataji miti na uchomaji wa mikaa kwa Wingi hapa Nchini.
Wakizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya mwenge wilayani Butiama mkaoni mara BW.Heikki Lindfors ambae ni Afisa uwandani( FIELD OPERATIONS)amesema kuwa lengo la kutengeneza mashine hiyo ni kuwawezesha watanzania kuepukana na utumiaji mikaa ambayo inaweza kuleta athari katika maeneo yao.
 ‘’ Inasaidia sana unapokuwa unatumia kwani tunawanawake ambao tumeanza nao wanaoka mikate kupitia mashine hii ambayo inatumia mionzi ya jua. Alisema.Bw,heikki lindfors.’’
Mashine hiyo haiathiri utumiaji wake kwani inasaidia kutoa ajira kwa kupitia vikundi ambavyo vitaundwa mpaka sasa wameaza na vikundi vitatu na baadae kuongeza hadi kufikia vikundi vitano na kudai kuwa lengo ni kuwafikia watanzania wote kwa lengo la kuondokana na utumiaji wa mikaa ili kuendelea kuifadhi Mistu.
 Mashine ya WARTSILA nikati ya mrandi ambao uko kwajiri ya kuwasidia watu ambao wakao katika kikundi na endapo utakamilika utasambazwa kwa wananchi.
Kwaupande wake kaimu mkurugenzi wa bodi ya Global Resource Alliance Tanzania Madaraka Nyerere amesema serikali kwa kushirikiana na taasisi za kifedha ili kuwawezesha vikundi hivyo kupata hizo mashine kwa lengo la kuanzisha miradi ya Bidhaa mbalimbali kwa kutumia jiko hilo.
Pia ameongeza kuwa ni vyema wanamara wakatumia fursa hiyo pindi itakapoanza kwa lengo la kupunguza utumiaji mikaa ili kuepuka kuathiri maisha yao kwani mashine hiyo ni nzuri na haliathiri kitu chochote kwa maisha ya binadamu.
Madaraka ameishukuru serikali kuazimisha siku ya mazingira wilayani Butiama kama mchango wa kumuenzi Baba wa Taifa hayati Mwl.julius Kambarage Nyerere na kitendo cha kupanda miti kwenye msitu wake nikama mmoja ya chachu kubwa ya kumuenzi.
Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni hifadhi mazingira mhimili wa Tanzania ya Viwanda.
Kote dunia mpaka sasa nizaidi ya Tani 9 zimeokolewa kutokana na uwepo wakifaa hicho kwani ukataji miti umepungua.
Aidha mkuu wa wilaya ya Butiama Bi.Annarose Nyamubi amewataka wananchi kujitokeza katika maadhimisho hayo ilikujifunza mambo mbalimbali kuhusiana na mazingira kutokana na maada ambazo zitakuwepo kwani kutakuwepo na kongamano litakalo husika najadili maada hizo.
    UNAWEZA KUTANGAZA NA MAKALIBLOG.
0754295996
      TUPE MAONI YAKO MATUSI HAPANA
Powered by Blogger.