Wakazi Wa Mwanza Waanza Kunufaika Na Efm Redio
Sehemu ya madereva bodaboda waliofika kupata mafuta bure katika Kituo cha mafuta cha Lake oil kilichopo mjini Mwanza- Kenyata Road
Sehemu ya magari binafsi yakionekana na stika ya 91.3 EFM yakisubiria kujazwa mafuta bure .
Piki piki zikiwa katika foleni ya kwa ajili ya kujaziwa mafuta.
Magazeti yalisomwa moja kwa moja kutoka Mwanza ( Kituo cha mabasi Igombe) na Maulidi wa Kitenge.
Mkazi wa mwanza akishuhudia pikipiki yake ikijaa mafuta
Sehemu ya timu ya Efm redio kwenye picha ya pamoja na mkuu wa Mkoa wa Mwanza mheshimiwa John Mongella baada ya kikao kifupi.
Timu ya Efm redio imetua rasmi katika mkoa wa Mwanza 91.3 fm ikiongozwa na Meneja mkuu ya Efm redio Denis Busulwa pamoja na Kitengena kuanza kuwawezesha wakazi wa Mkoa huo siku ya tarehe 05/06/2017, inatarajia kugawa mafuta bure katika vyombo vya moto (pikipiki, bajaji pamoja na magari) kwa kigezo cha kua na stika ya redio hiyo.
Efm redio imeleta furaha kubwa kwa madereva wa vyombo hususani madereva bodaboda wa mkoa huo kwani ni kitu ambacho hakijawahi tokea katika mkoa wao. Timu hiyo ya redio Efm inatarajia kupiga kambi katika mkoa huo kwa siku sita na inawaasa wasikilizaji wake kusikiliza kwa umakini redio ili waweze kupata taarifa ya mambo mazuri katika siku hizo pamoja na kujua ni wapi na mahali gani wataendelea kutoa mafuta.
Vilevile inatarajia kufanya jogging na wakazi wa mkoa huo kwa lengo la kuhamasisha jamii kufanya mazoezi ili kupunguza magonjwa yasioambukizwa.