Viongozi wa Kanisa la BapTisT Tarime watembelea Wagonjwa katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime Mkoani Mara na Hospitali ya Tarime Good Will Foundation Hospital kwa maombezi na wageni Kutoka U.S.A watoa msaada wa Vifaa vya kutunzia taka
Mkurugenzi wa Hospital ya Tarime Good Will Foundation Hospital Katikati Dkt Hudson Winani akikabidhiwa msaada wa vifaa vya kutunzia Taka kushoto wa kwanza ni Askofu Peter KasululuKanisa la Baptist jimbo la Tarime -Musoma kulia wa kwanza ni Joshua Theurer kutoka U.S.A
Dkt Hudson Winani akiongea na wageni kutoka U.S.A Walipotembelea hospital yake hii leo na kuwaombea wagonjwa pamoja na kutoa msaada wa vifaa vya kutunzia taka.
Dkt Hudson Winani akisalimiana na Mkuu wa Msafara Alisa Scher kutoka Hellen First Baptist iliyopo Nchini Marekani
Wageni walipotembelea chumba cha maabara
Kijana Nyitika Francis Miaka15 Mkazi wa Mutana kata ya Manga Wilayani Tarime Mkoani Mara akiombewa anasumbuliwa na Tumbo Kujaa gesi hata hivyo wageni hao wameweza kusaidia kijana huyo na kupelekwa hospital iliyopo Shirati ili kupewa matibabu zaidi kwa lengo la kunusuru maisha yake.
Kijana Nyitika Francis Miaka15 Mkazi wa Mutana kata ya Manga Wilayani Tarime Mkoani Mara akiwa amebebwa kwa ajili ya kupandishwa kwenye gari la kubeba wagonjwa ili ku[pelekwa Shirati kwa ajili ya Matibabu baada ya kusaidiwa na wageni hao kutoa U.S.A
Dkt Hudson winani katikati ni Askofu Peter Kasululu wakiwa na Alisia Scher Kutoka Hellen First Baptist U.S.A kwa lengo la kuzungumzia jinsi ya Kusaidia kijana Nyaitika Francis ambaye anasumbuliwa na tumbo.
Mchungaji Daud Christopher akisalimiana na mmoja wa wagonjwa katika Hospital ya Tarime Good Will Foundation Hospital.
Mganga Mkuu katika Hospital ya Halmashauri ya Mji wa Tarime Calvin Mwasha akiongea na wageni hao Ofisini kwake walipotermbelea hospitali hiyo na kutoa vifaa vya kutunza taka.
Mganga Mkuu Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Tarime Calvin Mwasha akiongea na wageni kutoka U.S.A Walipotembelea Hospitalini hapo kwa ajili ya kuombea wagonjwa na kutoa msaada wa vifaa vya kutunza taka.
Wakielekea maodini ili kuwaona wagonjwa kwa ajili ya maombezi.
Maombezi kwa wagonjwa katika Hospitali ya wilaya ya Tarime Mkoani Mara
Maombezi kwa wagonjwa katika Hospitali ya wilaya ya Tarime Mkoani Mara
Phales Yohana Buluma Muuguzi Kiongozi wa Wodi ya Watoto akielekeza wageni baada ya kutembelea wodi hiyo kwa ajili ya maombi.
Askofu wa kanisa la BapTisT Jimbo la Tarime -Musoma Peter Kasululu akikabidhi vifaa vya kutunzia taka katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime baada ya kutembelea eneoo hilo na kuwaombea wagonjwa
PICHA ZOTE NA CLEO24NEWS