UMOJA WA MAKANISA WAKABIDHI VIFAATIBA HOSPITALI YA MKOA WA SIMIYU.
![]() |
| Baadhi ya Viti vya kubebea wagonjwa(wheel chairs) vilivyotolewa na Shirika la Madhehebu ya Kikristo la Life Ministry kwa Hospitali Teule ya Mkoa wa Simiyu, mjini Bariadi. |
vifaa vilivyo tolewa
Life Ministry kwa
kushirikiana na umoja wa makanisa ya kikiristo mjini Bariadi wametoa vifaa tiba
ikiwemo baiskeli za kusukuma wagonjwa na vinginevyo vitakavyosaidia kutoa
huduma kwa mgonjwa aliyevunjika mifupa ambazo zimegharimu zaidi ya milioni 40.
Aidha Uhaba wa Vifaa
tiba katika Hospitali Teule ya Mkoa wa Simiyu (Somanda) bado ni changamoto
inayoikabili hospitali hiyo, hali inayofanya utoaji wa huduma za kitabibu kuwa
duni.
Akiongea kabla ya
kukabidhi vifaa tiba, Mkurugenzi wa Life Ministry Dismas Shekalaghe kwa
kushirikiana na umoja wa makanisa ya kikiristu Bariadi, amesema kuwa wanatoa
mchango huo ili kuipunguzia serikali mizigo ya bajeti katika mfuko wa
hospitali.
Amesema kuwa madaktari
na wauguzi wamekuwa wakiokoa maisha ya jamii katika kutoa matibabu na kanisa
pia huwa lina mchango wake katika jamii kwa watu wanaoishi.
‘’tuna vifaa kadhaa ambavyo tumeona tuvilete
hapa kama masaada tunashirikiana na umoja wa makanisa mkoa wa Simiyu…viti vya
kubebea wagonjwa, vifaa vya viuongo bandia, vifaa vya huduma ya meno, vifaa
vinavyotumika katika upasuaji, Bandeji na mabomba ya sindano zinafikia milioni 40 hadi 50’’
alisema Shekalaghe.
Aliongeza kuwa wanawashukuru Madaktari, Wauguzi
na manesi kwa kuokoa maisha ya watu wanaofika hospitali kupata matibabu ambao
wanafika hospitali kwa kukosa matibabu.
Akipokea Msaada huo kwa
niaba ya serikali, Mkuu wa mkoa wa Simiyu Antony Mtaka amesema kuwa katika
sekta ya afya hakuna msaada mdogo kwa sababu hata hicho kidogo kinaokoa maisha
ya watu.
Aidha Mtaka ameongeza
kuwa hospitali hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi lakini utatuzi wake ni wa
muda mrefu kwa kuwa bado ni mpya huku ikitegemewa na wananchi wengi
wanaoizunguka.
‘’tunashukuru kwa msaada
uliotolewa na life ministry utaisadia hospiatali hii pia iwawashawishi
madaktari kufanya kazi yao kwa ufanisi zaidi na ili
Madaktari na wauguzi waweze kutekeleza majukumu yao vizuri ni lazima wawezeshwe
vifaa, hivyo msaada huo utawatia moyo na kuongeza ari ya kufanya kazi.
Kwa upande wake Mganga
Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dr. Fredrick Mlekwa amesema kuwa msaada huyo
umewafikia kwa muda mwafaka kwa kuwa wako katikati ya bajeti, utawasadia katika
utoaji wa huduma kwa wananchi wanaofika kupata huduma hospitalini hapo.
“Tumefarijika sana kupata msaada huu na walengwa ambao ni
wananchi watapata huduma bora kupitia vifaa hivi, naomba nitoe wito kwa
Mashirika mengine ya madhehebu ya dini kuendelea kutusaidia kwa
kuwa Hospitali hii inawahudumia watu wenye mahitaji mbalimbali” alisema
Dkt.Mlekwa.
Nao baadhi ya wananchi
wameushukuru umoja wa makanisa huo kwa kuona mahitaji ya wagonjwa ambao ni
waumini wao, ambavyo vitasaidia wagonjwa wa aina yeyote hata wasio na dini ili
waweze kupata huduma hizo.
‘’vifaa hivi
vilivyotolwa na umoja huu wa makanis awatasaidia watu wote bila kujali itikadi
za dini zao, pia itakuwa ni hamsa kwa maktari na wauuguzi kufanya kazi kwa tija….alisema
Sylvester Sungwa mkazi wa Sima-Bariadi.
Na COSATNTINE MATHIAS SIMIYU





