TANESCO KUWAFIKIA WANANCHI MKOANI MARA;

Afisa mahusiano wa shirika la Umeme Tanzania TANESCO Mkoa wa Mara James Kuppa Vesso akionesha jinsi ya kutumia Umeme ambao unatumia njia Salama.( UMETA)
Baadhi ya wanachi waliofika katika banda la Shirika la hilo kupata Elimu Juu ya matumizi ya umeme na na Tahadhali zake katika maadhimisho ya siku ya mazingira  yanayofanyika kitaifa  mkoani Mara Wilayani Butiama.



wananchi wakipewa elimu.
Afisa mahusiano wa shirika la Umeme Tanzania TANESCO Mkoa wa Mara James Kuppa Vesso akiskilizwa kwa makini na wananchi waliokuwa wanapata elimu ya Utumiaji Umeme.

Mmoja ya wafanya kazi washirika hilo akitoa elimu 



Jinsi Umeme unavyosafiri hadi kumfikia mtumiaji vesso akineonesha



akizungumza na mwandishi wa Cleo24News




Shirika la umeme Tanzania Tanesco mkoani mara limewaomba wananchi kutumia fursa za shirika hilo ilikuondokana na uharibifu wa mazingira ikiwemo ukataji miti kwani mpaka sasa gharama zake nizachini ambapo  kila mwananchi anaweza kuzimudu.
Hayo yamebainishwa na  Afisa mahusiano wa shirika hilo mkoani Mara Bwana James Kuppa Vesso kipindi akizungumza na wandishi wa habari ambapo amesema kuwa mpaka sasa kwa wananchi wa vijijini wananunua umeme kwa bei nafuu ambapo kupitia siku ya mazingira wanatoa elimu ili kuelimisha njia wanayotoa umeme ambayo nisalama  na kila mwanachi anaweza kuimudu.
 “Mpaka sasa tumeboresha utoaji wa umeme kwa mwananchi hadi aliyeko kijijini gharama kwa UNIT 75 kuuzwa kwa Tsh 9150 lengo nikumuwezesha mwananchi ambae alikuwa amezoea kutumia kuni aweze kutumia umeme hata kupikia na siyo kuni ili kuondokana na uharibifu wa Mazingira alisema Vesso.
Hivyo kama wananchi watatumia fursa ambazo zinatolewa naTanesco itapunguza kwa kiasi kikubwa matumizi ya kuni jambo amabalo litasaidia kutunza misitu yetu.
Vesso amesema kuwa wataendelea kutoa elimu juu ya matumizi ya umeme ili wananchi kuondokana na utumiaji wamikaa ambapo wamekuwa wakitoelimu kwa kupitia majarida vyombo vya habari na maonesho mbalimbali ambayo yanayofanyika katika maeneo husika.
HAKIKA TANESCO TUNAANGAZA MAISHA YAKO.

TANGAZA  NA MAKALINEWS; 0754295996
TUPE MAONI YAKO MATUSI HAPANA;

Powered by Blogger.