TANESCO MKOANI MARA KUENDELEA KUPELEKA NEEMA VIJIJINI;

wafanya kazi wa shirika la umeme Tanzania TANESCO MKOANI MARA Wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa maadhimisho ya siku ya mazingira
WAFNYA KAZI HAO  MMOJA YA KAZI YAO KATIKA MAONYESHO WANAVYO FANYA KAZI
 


Mmoja ya wataalamu wa TANESCO  Akitoa maelezo kwa wananchi jinsi umeme unavyozalishwa, kusafirishwankusambazwa hadi kumfiki mteja ambayo  ni hatua ya mwisho ya matumizi.


 WANANCHI WAKIMFATILIA VIZURI MFANYA KAZI WA SHIRIKA HILO ALIVOKUWA AKITOA MAELEKEZO.
Shirika la umeme Tanzania TANESCO Mkoani Mara limesema litashirikiana na wananchi kuwapa huduma bora kutokana na kuendelea kuboresha huduma zao kila kukicha.

Aliyasema hayo Bwana Vesso ambae ni Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja mkoani Mara na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano wa karibu kila wanapopata matatizo katika maeneo yao, ambapo alisema wakati umefika kwa wananchi kuacha kuharibu mazingira kwani TANESCO wamejizatiti kundoa kero ya ukosefu wa umeme hapa nchini.

Pia aliongeza na kusema mpaka sasa upatikanaji wa umeme viijini mkoani Mara uko vizuri,vilevile gharama ya unit kwa wateja wa vijijini walio katika miradi ya REA ni nafuu kwani wanaweza kupata unit 75 kwa gharama ya Tshs 9,150/- ambapo bei hii ya kiwango cha chini inayoweza kumpa unafuu mtumiaji wa huduma ya umeme na kuepukana na uharibifu wa mazingira kwa kukata miti kwa ajili ya kuni na matumizi mengine.
 Aliongeza na kusema lengo la shirika ni kuwafikia watumiaji popote walipo.

Aidha amewataka wakazi wa mkoa wa Mara kuchangamkia fursa ya matumizi ya kifaa cha  UMETA unatumika kama mbadala ya udandazaji wa mifumo ya waya ndani ya nyumba kwa wateja wenye chumba kimoja hadi viwili. 

Bwana Vesso  aliongeza kwa kusema fursa hii yaweza kutumika kwa ajili ya kuendesha mitambo midogo midogo ya umeme wa njia moja zikiwemo salon,maduka ya vinywaji,kutengenezea juice n,k.

Ujio wa UMETA ni fursa bora kwa wananchi wa Tanzania na inaweza kusaidia kuondoa tatizo la ajira katika maeneo yote ya nchini kwani kila mtu anao uwezo wakutumia kifaa hicho kufungua biashara ngodo na kujiajiri.

James Vesso amesema kuwa ataendelea kutoa elimu kwa wananchi ilikutumia neema kama hizi zinazojitokeza katika mkoa wa Mara.

Nami mwandishi wa makaliblog nakamilisha kwa kusema Hongereni TANESCO lakini jaribuni kwenda zaidi vijijini ambako lipo wimbi la vijana waliokosa ajira lakini kwa kupitia umeme huu usiotumia wayaring utawasidia kufungua ofisi zao na kujipata kipato na pengine kusaidia familia zao kwa kujipatia mlo wa mara tatu kupitia mawazo yenu mliyoaanzisha.


UNAWEZA KUTANGAZA NASI TUPIGIE KWENYE
                    0754295996
Powered by Blogger.