Manchester United YAANZA SAFARI YAKUMRUDISHA RONALDO Old Trafford.
Hakuna ajuae hili movie litaisha lini kwani kila msimu wa
usajili linaibuka, baada ya Ronaldo kusema hataki tena kuendelea kucheza
soka nchini Hispania, klabu ya Manchester United wameibuka upyaa na
inasemekana wanataka kumrudisha Old Trafford.
Vyanzo mbalimbali vya habari vimesema Manchester United
wanataka kujaribu kutuma ofa kwa Real Madrid kuona kama wanaweza
kukubali kumuuza mwanasoka bora huyo wa dunia mwenye umri wa miaka 31.
Pamoja na vilabu kama PSG na baadhi ya timu kutoka Marekani
na China kumtaka mchezaji huyo lakini hakika Ronaldo atapenda kuona ofa
ya Manchester United mezani kwa Real Madrid kwa kuwa hapo ndio
anapopapenda.
Lakini gazeti la Marca linasema kocha wa Real Madrid
Zinedine Zidane hayuko tayari kumuona Ronaldo anaondoka Real Madrid na
tayari ameshaanza kufanya mpango wa kuongea naye kuhusu kubaki Santiago
Bernabeu.
Usajili wa Ronaldo kwenda Real Madrid bado unaweza kuwa na
vikwazo vingi kwani Real Madrid toka dirisha hili la usajili lianze
wanaonekana kuwawekea vikwazo United katika suala la kununua wachezaji
wao.
Kama unakumbuka Unitec wameshajaribu kumnunua Bale
ikashindikana na sasa wamewekewa kiwingu katika usajili wa Alvaro Morata
na James Rodriguez ambao wote wanawataka.