ASKOFU SANGU ATOA CHOZI BAADA YA KUTEMBELEA KANISA LILILOPOTEZA MAISHA WAUMINI WALIOKUWA WAKIJIKINGA MVUA.
Askofu Lieberatus sangu akaangalia ukuta uliokuwa umeawaangukia waumi na kusababisha vifo.
Askofu Liberatus Sangu akibariki moja ya makaburi walimozikwa waumini baada ya kuangukiwa na ukuta wa kanisa.
Askofu Liberatus Sangu akiwa na majeruhi wa tukio hilo, kulia kwake ni paroko wa parokia ya Ilumya Padri.
ASKOFU wa Kanisa la Romani katoliki jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu amezulu eneo la kanisa na kububujikwa na machozi mara baada ya kuona eneo na ukuta wa kanisa ulioanguka na kuuwa waumini wakati wakijikinga mvua.
Kanisa hilo lko kijiji cha Lubugu wilaya ya Magu mkoani Mwanza liliwaangukia waumini wa kanisa hilo wakati wakiwa katika ibada wakati wa mvua iliyokuwa imeambatana na upepo miezi michache iliyopita.
Katika tukio hilo la kuanguka kwa kanisa wakati waumini wakiendelea na misa ni watu wawili walipoteza maisha na wengine kujeruhiwa na hata kusababishiwa kupata ulemavu wa kudumu.
Askofu alisema kuwa waliokufa katika ajali hiyo ya kuanguka kwa kanisa ni washindi wa vita kwani ni wachache wanaokufa wakiwa katika matukio ya kimungu,wengi wamekuwa wakipoteza maisha katika virabu vya pombe na sehemu ambazo ni za sitarehe,akiwatolea mifano waliokufa wakiwa katika ibada ni Wamisionari pugu,Romeru huko marekani na padre James Sangu aliyekufa akiendesha misa.
“Mungu nakuomba hata mimi uweze kunichukua nikiwa katikanyumba ya ibada kama ulivyo wachukua waumini hao ambao alisema si vyema kuwataja majina yao”
Aidha aliongeza kuwa anawapa pole wale wote walionusulika katika ajali hiyo na kuwataka kutoteteleka katika imani kwani hiyo ni mipango ya Mungu na hapa duniani kuna kila aina ya majaribu kwa watu wa Mungu,hivyo msikate tama katika kumuomba Mungu.
Askofu Sangu alifanya sara maalumu na kisha kutembelea mahali walipohifadhiwa waumini hao ambako anasema kuwa alimwagiza paroko watu hao wazikwe karibu na kanisa ili kuonyesha ni jinsi gani walivyo washindi katika kupambana na shetani.
Aidha aliwataja walionusurika katika ajali hiyo ni Petro Mapindi katkista,Jesca Petro (darasa la pili) aliyevunjika miguu yote ingawa kwa sasa anaendelea vizuri,Sabina Magadula(72) na Sara Timotheo ambaye ni mwanafuzi wa darasa la pili katika shule ya msingi Lubugu.
Bi, Sabina Magadula(72) ni mmoja wa wahanga waliopona katika ajali hiyo anasema kuwa ilikuwa ni kama mchezo lakini kumbe ndio ilivyotokea kwa kuwapoteza wenzetu na sie kubaki.
Niliumia sana na wala sikutarajia kama naweza kupona lakini kwa mipango ya Mungu niko hai na ninaendelea na kazi zangu za kila siku ila cha msingi ni kumwamini Mungu tu kwani hapa duniani yote yanawezekana Alisema.
Kwa upande wake Petro Mapindi(56) ambaye ni katikista wa kanisa hilo la Lubugu na pia ni muhanga wa tukio hilo anaeleza kuwa ni mvua na upepo mkali uliokuwa ukiambatana na kibumga kikali ndicho kilichokuwa chanzo cha kuanguka kwa kanisa hilo.
“Anaeleza kuwa upepo mkali na mvua ya kawaida ilionekana lakini kutokana na uimara wa kanisa lao awakuwa na wasiwasi wowote ule lakini Ghafla niliona matofari yakishuka kwa kasi na upepo wa kimbunga nafumbua macho nikamuona padre amezungukwa na matofari nilikimbia kwenda kumuokoa na kumtoa nje”
Aliongeza kuwa mara baada ya tukio hilo la kuwaokoa waumini wenzangu nilitafuta gari na kuwakimbiza katika hospitali ya magu,ingawa mtoto mmoja wa kike alifia hapo hapo na mwingine mama alifia mlangoni mwa hospitali.
Kwa upande wake padre wa parokia hiyo ya Ilumya Michael Kumalija alisema kuwa tukio hilo lilisemwa na mambo mengi lakini Mungu ni mwema waumini awaweza kuteteleka juu ya maneno ya mitaani.
Aliongeza kuwa hata yeye akujua la kufanya ila alijishitukia yuko nje na anapewa msaada na waumini wake,hivyo kila jambo linamkono wa mungu na kwa kuwa nlilikwisha pita basi sisi tunaangalia ujenzi upya wa kanisa katika eneo hilo Alisema Kumalija.
NA MAKALIBLOG;
TANGAZA NASI KUPITIA 0754295996. POPOTE ULIPO
TUPE MAONI YAKO MATUSI( HAPANA)