PROFESA MHONGO AWATAKA WANANCHI WAKE KUENDELEA NA SHUGHULI ZAO WALIZO ZIPANGA ZA MAENDELEO JIMBONI KWAKE;

[​IMG]
 NA Mwandishi wa MAKALIBLOG.MARA
Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Profesa Sospeter Muhongo amewataka wananchi wa Jimbo  lake  kuhakikisha wanaendelea  na mipango yao ya shughuli zote za maendeleo  ikiwa na ujenzi wa vyumba vya  madarasa kama walivyokubaliana na kusahau yote yaliyotokea.
Akizungumza na waandishi wa habari Katibu wa Mbunge Juma Ramadhani alisema kuwa wananchi wa Jimbo hilo wanatakiwa kusahau yote yaliyotokea kwa mbunge wao na,kwamba kazi iliyoko mbele yao ni ujenzi wa vyumba vya  madarasa pamoja na mipango mingine ya maendeleo waliyokuwa wamekwisha ipanga katika jimbo lao.

“kazi iliyoko mbele yetu ni ujenzi wa madarasa  na kadhalika,malengo yetu ni yaleyale na kasi ni ileile hakijaharibika chochote,hivyo tujipange kwa ajili ya maendeleo ya Jimbo letu”alisema Katibu huyo.
Ramadhani alisema  kuwa mbunge huyo pia amewataka viongozi na wananchi wa jimbo hilo kujituma zaidi na kwa kasi zaidi katika maeneo yao ndani ya vijiji na kata ili kuendelea na shughuli  ujenzi wa Taifa.

Mmoja wananchi wa Jimbo hilo nyasatu mafuru alisema kwa masikitiko kwa  tukio la kutenguliwa kwa nafasi ya Uwaziri wa Nishati na Madini mbunge wao,limewashitua sana lakini wanachofahamu ni kwamba hata kama ameondolewa kwenye nafasi hiyo shughuli zao za maendeleo zitaendelea kama kawaida na kama alivyokuwa amekwisha anza kutekeleza ahadi zake.

        NA MAKALIBLOG MARA.
Powered by Blogger.