MAKAMU WA RAIS MHE; SAMIA SULUHU HASAN KUFANYA ZIARA MKOANI MARA SIKU YA MAZINGIRA;
![Image result for MAMA SAMIA KATIKA MIKUTANO MBALIMBALI](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgKX56mwanI2ROh0cJHscJZwvWDlZyiFNMBpp-dmX0ab0zFezpj8o4-GDihRt__xw-lhS5S7tYPqKTa13GpZNXPqqBqV_Zy2gmSWnMO6og5GTspDFjofqdHkjSHwMcp_wb0-bxYTirEOnM/s640/11.jpg)
Na MAKALIBLOG. MARA
MKUU wa Mkoa wa Mara Dk. Charles Mlingwa amesema kuwa watatumia fursa ya
siku ya maadhimisho ya Mazingira itakayofanyika katika wilaya ya
Butiama Mkoani humo kuielimisha jamii ili kuweza kukabiliana na changamoto ya
uharibifu wa mazingira
hususani uoto wa asili ambao umetoweka kwa
ajili ya wa kukata miti ovyo mkoa wa Mara.
Ameyasema hayo wakati akitoa taarifa ya siku ya maadhimisho ya
mazingira Duniani ambayo kitaifa inafanyika katika Wilaya ya Butiama
waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari katika ukumbi wa
Uwekezaji uliopo ofisi ya Mkuu wa mkoa itakayofanyika katika wilaya ya
Butiama Mkoani hapa.
Dk. Mlingwa alisema kuwa maadhimisho hayo ambayo huadhimishwa kuanzia
tarehe 1- 5 mwezi Juni kila mwaka yatafunguliwa na Juni 1 mwaka
huu katika viwanja vya Mwenge Wilaya ya Butiama ambapo Makamu wa
Rais Samia suhulu Hassan atakuwa Mgeni rasmi katika kilele cha
maadhimisho hayo na kufunguliwa Juni Mosi na Waziri wa Ncbi, Ofisi ya
Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira, January Makamba.
Aliongeza kuwa maadhimisho hayo yatafuatana na kongamano
linalohusiana na masuala ya mazingira ikiwa ni pamoja na upandaji wa
miche ya asili ipatayo 1,500 katika msitu wa Baba wa Taifa ili
kuenzi kazi zote katika hifadhi ya mazingira .
Alizitaja faida ambazo mkoa huo utazipata kupitia fursa hiyo ya
maadhimisho kuwa ni pamoja na kuwajengea jamii uwezo juu ya uelewa
wa masula ya utunzaji wa mazingira na changamoto za kijamii
zinazojitokeza katika utunzaji wa mazingira,kuwawezesha wadau
kushiriki katika fursa zinazohusiana na upandaji wa miti na kujadili
mwendelezo wa utekelezaji wa shughuli zilizoratibiwa katika mkoa na
wizara kuhusu namna bora ya uhifadhi wa mazingira.
Nyingine ni kuelimisha wananchi kupanda miti ili kukidhi mahitaji
ya dunia kupambana na ongezeko la hewa ya carbon Dioxide(ukaa)na
kuenzi kazi zote za Baba wa Taifa Mwl. Nyerere katika utekelezaji
wa maendeleo hususani katika hifadhi ya mazingira
NA MAKALIBLO. MARA;
TUPE MAONI YAKO MATUSI HAPANA