SAFARI YA KUMUUNGA MKONO RAIS KUHUSU VIWANDA MARA YATANGULIA MWEKEZAJI MoU ASAIN KUJENGA KIWANDA CHA SUKARI
Uchumi wa viwanda: Safari ya kuanzisha viwanda
katika Wilaya ya Tarime imeanza rasmi leo baada ya kampuni ya Nile Agro
Industries Limited ya Uganda kusaini Makubaliano(MoU) ya kujenga kiwanda cha sukari Wilayani Tarime.
Hafla ya kusaini makubaliano hayo imefanyika leo
katika ukumbi wa uwekezaji katika ofisi
ya Mkuu wa Mkoa wa Mara na kushuhudiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mara Dkt Charles
Mlingwa, viongozi wa jamii kutoka vijiji vinavyotegemea kunufaika na uwekezaji
huo, wafanyabiashara wakiwemo wakandarasi wa Wilaya ya Tarime.
Akitaja faida za uwekezaji huo, Mkuu wa Wilaya ya
Tarime Glorious Luoga amesema ujenzi wa kiwanda hicho utatoa ajira (direct employment)
5,000, na indirect employment kwa watu
10,000 pamoja na kusadia wakulima
kuanzisha kilimo cha miwa kama zao lao la biashara.
DC Luoga uwekezaji huo utaiwezesha pia Halmashauri
ya Wilaya ya Tarime kuongeza mapato yake kupitia ushuru wa huduma na kodi zingine
zitakazokuwa zikilipewa serikari kuu.
“ Uwekezaji huu utabadilisha Tarime na Mara kilimo cha miwa itakuwa dhahabu isiyoisha”,
amesema Luoga na kuongeza kuwa tayari
kuna eneo lenye ukubwa wa hekta 4439 ambalo liko tayari kwa ajili ya uwekezaji
huo na hekta zingine 1,297 kwa ajili ya wakulima wadogowadogo.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mara Dkt Mlingwa amemkaribisha mwekezaji huyo na kumuahidi
ushirikiano wa kutosha.
Dkt Mlingwa amempongeza pia Mkuu wa Wilaya ya Tarime
kwa juhudi ambazo amefanya kuanzishaji wa kilimo cha miwa na kiwanda cha
sukari.
“ Kwa namna ya pekee kabisa nakupongeza Mkuu wa Wilaya
ya Tarime (Luoga) na timu yako kwa
kufikia hatua hii”, amesema RC Mlingwa.
Akiongea baada ya kusaini makubaliano hayo
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Tarime Moses Misiwa amesema ujio wa
mwekezaji huyo ni neema kubwa kwa wanatarime na kusema kuwa wamejipanga vizuri
kuhakikisha uwekezaji huo unakuwa na mfanikio makubwa.
Mwenyekiti wa Nile Agro Industruries Limited Patel
Magan na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Patel Gajendra wameshiriki kusaini makubaliano hayo
na kusema wako tayari kujenga kiwanda hicho bila kuchelewa.
RC Mlingwa akizungumza katika hafla hiyo |
Mkuu wa Wilaya ya Tarime Glorious Luoga akitaja faida zitakazotokana na uwekezaji wa kiwanda cha sukari |
Picha ya pamoja baada makubaliano ya kujenga kiwanda cha sukari katika Wilaya ya Tarime |