MASHABIKI WA YANGA AFRICA WASABABISHA TIMU YAO KUPIGWA BARUA YA ONYO;
Baada
ya Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi Tanzania au Kamati ya Saa
72, kufanya kikako chake, imetaka Yanga ipewe onyo baada ya mashabiki
wake kumwaga maji vyumbani.
Mechi namba 195 (Yanga 1 vs Azam 0). Yanga
haikuingia kwenye chumba chake cha kubadilishia nguo, kutokana na kuwa
na maji yaliyomwagwa na wanachama wa klabu hiyo (makomandoo) muda mfupi
kabla ya timu hiyo kuwasili uwanjani.
Kamati
imeelekeza klabu ya Yanga iandikiwe barua ya onyo, na kuitaka
kuhakikisha wanachama wake wanaacha mara moja mtindo wa kumwaga maji
vyumbani baada ya kuwa vimeshafanyiwa usafi na wafanyakazi wa uwanja
tayari kwa ajili ya matumizi ya timu yao.
PICHA NA SALEHEJEMBE.