Nyoka apatikana kwenye ndege Marekani



 Nyoka

Nyoka amegunduliwa kwenye ndege iliyokuwa safarini kuelekea mji wa Anchorage katika jimbo la Alaska Marekani.

Taarifa zinasema nyoka huyo aliachwa kwenye ndege hiyo na abiria.
Alikuwa ameorodheshwa kama 'mnyama kipenzi' na abiria huyo katika safari nyingine iliyokuwa imefanywa na ndege hiyo.
Abiria walifahamishwa kuhusu uwepo wa nyoka huyo rubani alipotangaza: "Jamaa, tuna nyoka ndani ya ndege hii, lakini hatujafahamu yuko wapi hasa."
Nyoka huyo wa futi tano hakuwa na sumu na alionekana mara ya kwanza kwenye ndege na mvulana alikuwa amepanda na kusimama juu ya kiti.
snake in a bag
Mvulana huyo alipomuona nyoka huyo, nyoka huyo alikuwa amelala na kufunikwa kiasi na begi.
Kwa mujibu wa mamake mvulana huyo, Anna McConnaughy, hakukutokea mtafaruku kwenye ndege hiyo.
Wahudumu wa ndege walimchukua nyoka huyo na kumfungia ndani ya mfuko wa plastiki wa kukusanyia taka.
Aliwekwa kwenye sehemu ya kuhifadhia taka kwenye ndege hadi ndege hiyo ilipowasili kwenye uwanja wa ndege Anchorage.

Wahudumu walifahamu kuhusu nyoka huyo mara ya kwanza abiria alipopiga ripoti kwamba alikuwa amempoteza mnyama kipenzi wake akiwa safarini kwenda Aniak katika jimbo la Alaska.
Alidokeza kwamba huenda mnyama huyo wake alikuwa kwenye ndege iliyokuwa safarini kurejea Anchorage.
Powered by Blogger.