NIMEKUWEKEA STORY NA MATUKIO SIKU YA SHERIA MUSOMA;
Kufuatia gharama za kufungulia mashauri katika mabaraza ya aridhi na nyumba kuwa kubwa,kunachangia
kukithiri kwa migogoro ya kijamii isiyoisha na mauaji ya kinyama na kisasi,imeelezwa.
Hayo yalielezwa na mwanasheria mwandamizi kutoka chama cha
mawakili wa Tanganyika(TLS) Ostack Mligo wakati akihutubia kwenye mkutano wa
maadhimisho ya siku ya sheria nchini,katika viwanja vya mahakama ya Mkoa wa
Mara mjini Musoma jana.
Mligo alisema kutokana na gharama za kufungua mashauri katika
mahakama zote kuwa kubwa kulingana na thamani ya mali,zimekuwa zikiwafanya
wananchi walio na kipato cha chini kutofungua mashauri kwa kukosa ada za
kulipia mahakamani,na kuishia kupambana katika ngazi za kifamiliya na koo.
Alisema kwa kuwa serikali inazungumzia usikilizwaji wa mashauri
kwa muda mfupi kwa lengo la kukuza uchumi ni vema wakaangalia gharama za
ufunguaji wa mashauri ili kila mwananchi mwenye tatizo awe na uwezo wa kuzimudu
.
Kwa upande wake hakimu
mkazi mfawidhi,kaimu hakimu wa mkoa Karimu Mushi alisema katika kutoa
maamuzi ya mashauri mbalimbali kumekuwepo na changamoto za kisheria na wadau
ambazo ni vifungu vya sheria namba 98 na 225 vya sheria za mwenendo wa jinai.
Mushi alisema vifungu hivyo havielezi ukomo wa upande wa
mashtaka kurudisha shauri mahakamani pale linapokuwa limefutwa ama kuondolewa
kutokana na kukosekana kwa ushahidi,na kwamba upande wa mashtaka unao uwezo wa
kurudisha shauri hilo mahakamani zaidi ya mara kumi,jambo ambalo limekuwa
likiwachanganya walalamikiwa.
Alisema kufuatia adha hiyo walalamikiwa wamekuwa wakipoteza
muda mwingi kuhudhuria mahakamani na kushindwa kushiriki kikamilifu katika
shughuli za ukusji wa uchumi.
Kwa upande wake mgeni rasmi kaimu Mkuu wa Mkoa,ambae ni Mkuu
wa Wilaya ya Musoma Dkt. Vicent Naano alisema katika kusimamia sheria serikali
na mahakama zinategemeana na ndio maana serikali inahimiza mashauri yamalizike
kwa wakati ili wananchi waweze kufanya shufhuli za kujiingizia kipato na kukuza
pato la taifa.
Dkt.Naano alisema atahakikisha mapungufu yaliyotajwa
anayafanyia kazi na majibu yake kuonekana ili kuweza kumaliza dosari zitokanazo
na muhimili wa sheria ikiwa ni pamoja na kusogeza huduma ya mahakama ya aridhi na
nyumba karibu na wananchi .