Kutokana na ukame ambao umeashamili maeneo mbalimbali ya
Nchi na kupelekea baadhi ya vyanzo vya maji kukauka Hospitali ya Wilaya ya Tarime Mkoani Mara imekumbwa
na changamoto ya ukosefu wa maji jambo ambalo limemusukuma Mwenyekiti wa Bodi
ya ukarabati wa Hospital hiyo Peter Zacharia kutoa Gari kwa ajili ya kuleta Maji kwa lengo la kutatua changamoto
hiyo.
Zacharia ambaye ni mdau wa maendeleo pia Mwenyekiti wa
kamati ya ukarabati wa Hospital hiyo na
mfanyabiashara amesema kuwa ameamua kutoa msaada huo wa gari la kusomba maji
ili kutatua changamoto ya ukosefu wa maji katika hospital hiyo kwani wagonjwa
wamekuwa wakiteseka kwa sababu ya ukosefu wa maji.
“Nikiwa tumboni mwa
mama yangu na nilipozaliwa nilijaliwa na mwenyezi Mungu kuwa injinia wa mambo
mbalimbali na sasa nausika na magari ya usafirishaji sasa wanachi wa Tarime
ninachowalaumu hawataki maendeleo na wanapinga sana mtu ambaye anataka
kuwasaidia wanachagua viongozi ambao wanajali posho na maslahi yao tu” alisema
Zacharia.
Akipokea Msaada wa maji hayo Matron wa Hospital hiyo Paulina
Shirole ametoa shukrani zake na kudai kuwa kipindi cha nyuma takribani wiki
moja suala zima la maji limekuwa changmoto kubwa na kupelekea suala zima la
usafi kukwama.
Nao baadhi ya wanachi ambao wanauguza katika Hospital hiyo wametoa
shukrani zao kutokana na msaada huo huku wakizungumzia hadha waliokuwa wikipata
kipindi cha Nyuma kuwa baadhi huduma zimekuiwa zikikwama kwa sababu ya ukkosefu
wa maji
|