Yanga kuilipa Simba milioni 200 kwa ajili ya Kessy
Yanga imekubali kuilipa Simba Sh milioni 200 kumaliza utata wa Hassan Kessy kudaiwa kuvunja mkataba na klabu yake ya zamani Simba.
Yanga kuilipa Simba milioni 200 kwa ajili ya Kessy
Awali, Simba
ilimlalamikia mchezaji Hassan Kessy kwa kuvunja mkataba na kudai kulipwa
thamani ya mkataba ambayo ni zaidi ya dola laki sita, lakini baada ya
mazungumzo Yanga wamekubali kulipa asilimia 10 ya mkataba.
Ofisa Habari wa
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) amesema Yanga iliwakilishwa na Kaimu
Katibu Mkuu, Baraka Deusdedit na Simba iliwasilishwa na Mwenyekiti wa
Kamati ya Usajili, Zacharia Hanspope.
Lucas alisema
walikubaliana kufika kikomo wikiendi hii kwa muda na sehemu wanayoijua
wao ili waweze kumalizana kabisa kwa sababu wamekubaliana kuwekeza
sehemu ili kulipa fidia na kumaliza utata wa kile ambacho Simba imekuwa
ikikilalamikia.
Ili kuepuka suala hili
kurudi kwenye kamati ya Sheria na hadhi za wachezaji hawa viongozi
wamekubali kumaliza na kuandika ripoti na kuileta TFF Jumatatu.
Awali Simba ilipeleka
shauri kwenye Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji kuwa
mchezaji Hassan Kessy Juni 27 mwaka huu alivunja mkataba kwa kitendo cha
kuonekana akiwa na timu ya Yanga ilihali mkataba wake ukiwa
haujamalizika Simba.
Kamati baada ya kupokea
shauri hilo iliagiza pande za Simba na Yanga kumaliza suala hilo tangu
Septemba, lakini kwa sababu zilizo nje ya TFF na kamati kuamua kulipa
msuluhishi ambaye alikuwa ni Said El-Maamry.