WANDISHI MKOANI MARA WAWEZESHWA;
Na Ada Ouko,Musoma.
CHAMA cha ushirika akiba na mikopo Imara Saccos mjini Musoma
kimeanzisha mfuko maalum kwa waandishi wa habari wajasiriamali mkoa wa Mara ili
kuwasaidia kukopa fedha zitakazowawezesha kununua vitendea kazi na kufanya
shughuli zao kwa ufanisi sambamba na hilo kutoa elimu ya ujasiriamali kwa wananchi.
Ufunguzi wa mfuko huo ulifanyika baada ya viongozi wa chama
hicho kufanya kikao cha bodi ambapo walikubaliana kuanzisha mfuko huo na mifuko
mingine ya kijamii kama mfuko wa wanawake ambao ni wajasiriamali wadogo mfuko
wa wajasiriamali vijana pamoja na mfuko wa wazee waliostaafu kazi.
Kauli hiyo ilitolewa hivi karibuni na mwenyekiti wa chama
hicho Boniphace Ndengo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake
alisema mfuko wa wajasiriamali waandishi wa habari utawawezesha kununua nyenzo na
zana zitakazo wasaidia kufanya shughuli zao ili wapate maendeleo binafsi na
kukuza uchumi wa taifa.
‘’Tunafikiria kuongeza pesa kila wakati lakini kwa sasa tumeanza
na milioni 2 hatuwezi kusubiri tupate pesa nyingi hizohizo kidogo tunazigawa
ili tupate mtaji kwa hiyo hizi pesa zitakuwepo pale ilikuwezesha waandishi wa
habari kununua vifaa vya kazi zao pia kutoa elimu ya ujasiriamali kwa
wafanyabiashara wadogowadogo ili kukuza uchumi wao ‘’alisema.
Alisema ili kukopa katika mfuko huo lazima mwandishi wa
habari aweze kutimiza masharti ambayo ni kuchangia shilingi 50,000 au zaidi
kabla ya kuomba mkopo pesa itakayotolewa kila mwezi kwa miezi sita ataruhusiwa
kuchukua mkopo ambao utatolewa na kurejeshwa bila riba,kiasi hicho cha fedha
kitawezesha kukua kwa mfuko huo hatimaye kuwawekea akiba.
‘’Ili kufanya mfuko ule
kuwa mali yenu ni kwamba ile michango mtakayoitoa sisi tutaifanya kama
hisa ili kusudi mfuko ukiwa na fedha ya ziada tunaweza kutoa hiyo ziada
tuwalipe wana hisa wa mfuko maana yake kama mtu ajachangia hatakuwa na hisa pia
hataweza kupewa mkopo’’alisema.
Ndengo aliwataka waandishi hao kuchagua kiongozi ambaye
watamuamini ili kusimamia mfuko huo jambo ambalo walikataa na kusema kwakuwa
chama hicho ndio kimewafungulia mfuko huo basi pia wawezekuwasaidia kuusimamia
wenyewe.
Agostino Mgendi ni
miongoni mwa waandishi hao alishukuru kwa niaba ya wenzake alitaka kujua
marejesho yanafanyikaje baada ya kukopa pia kwa dharula ya kiafya kwani waandishi hao wanatumia bima
ya afya ambapo alijibiwa na mwenyekiti huyo kuwa fedha inayotolewa lazima
ielezwe matumizi yake sambamba na hilo dharula itatolewa na kama kuna
changamoto ya uchumi watasikilizwa.
Mwisho.