tuzo za EATV, kufanyika 12 Desemba
Tuzo
za EATV zimeanzishwa mwaka 2016 na kampuni ya East Africa Television na
Radio, zitafanyika kwa mara ya kwanza tarehe 10/12/2016 jijini Dar Es
Salaam,Tanzania.
Tuzo
hizi zinashirikisha wasanii wa muziki na filamu kutoka nchi za Afrika
Mashariki na zitakuwa zikifanyika kila mwaka, huku vipengele vya tuzo
vikiongezeka kila mwaka kutoka vipengele kumi vinavyoshindaniwa mwaka
huu.
Kuanzishwa
kwa tuzo hizi kuna lengo la kuthamini wasanii na kuleta ushindani
kwenye sekta hii ya sanaa kwenye ukanda huu wa Afrika Mashariki.
Kwenye
tuzo za mwaka huu kutakuwepo na jumla ya vipengele kumi. Vipengele sita
vitashindaniwa na wasanii wa muziki, Vipengele vitatu vitashindaniwa na
wasanii wa filamu na kipengele kimoja kitakua ni tuzo ya heshima.
Vipengele
hivyo kwa upande wa muziki ni mwanamuziki bora wa kiume, mwanamuziki
bora wa kike, mwanamuziki bora Chipukizi, kundi bora la mwaka, Video
bora ya mwaka na Wimbo bora wa mwaka.
Kwa upande wa Filamu vipengele vitakavyoshindaniwa ni Filamu bora ya Mwaka, Muigizaji Bora wa Kiume na Muigizaji Bora wa kike.
Tuzo za EATV 2016 zinafanyika kwa udhamini wa Coca Cola na Vodacom Tanzania.