ASKARI POLISI WATATU WAFUKUZWA KAZI MWANZA KWA UTOVU WA NIDHAMU NA RUSHWA

Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza limewafukuza kazi askari watatu kwa tuhuma za kukiuka maadili ya kazi ikiwemo kujihusisha na vitendo vya utovu wa nidhamu pamoja na upokeaji wa rushwa.


Akizungumza na askari hao Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema kuwa hatua imechukuliwa ili iwe fundisho kwa askari wengine wanaokwenda kinyume na maadili ya kazi hiyo.


Amesema askari mmoja kati ya hao alikutwa akiwa amelewa na kulala lindoni, huku wengine wawili wakituhumiwa kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu.


Kamanda Msanga amesema ukiukwaji wa maadili ni chanzo cha ongezeko la uhalifu hivyo hatamvumilia askari yoyote atakaye kwenda kinyume kwa kuwa kwa kufanya hivyo kunalichafulia hadhi jeshi la polisi kwa sababu ya makosa ya askari wachache.


Kamanda Msingi ametumia nafasi hiyo kuwakumbusha askari kufuata weledi wa kazi zao na kusema askari wanaotumia vyeo vyao kwa ajili ya kujipatia pesa kutoka kwa wananchi atawatumbua kabla kasi hiyo ya utumbuaji haijamfikia kwa kushindwa kuwasimamia.
Powered by Blogger.