UMATI YA KABIDHI SHILINGI MILION TANO KWA WASICHANA WALIOPATA MIMBA CHINI YA UMRI WAMIAKA KUMI NANANE ILIKUWAINUA KIUCHUMI

 ANGALIA PICHA ZA MATUKIO YOTE YA MAFUNZO YA UMATI NA WAKATI WAKUKABIDHI FEDHA KWA WALENGWA.

meneja mradi kanda UMAT bw nyangwengwe WANGO akimkabidhi fedha  kwa bintia ambae yeye alizaa akiwa na umri mdogo baada ya mafunzo ya kuzitambua fursa zinazowazunguka nakuwainua kiuchumi mabinti hao ambao wako katika mazingira  hatarishi.
 















Zaidi ya shilingi milioni 5 zimetolewa kwa wasichana waliopata mimba chini ya umri wamika kumi nanane ilikuwawezesha kuwakomboa  kiuchumi kutokana na fursa zinazowazunguka fedha hizo zimetolewa na UMAT kwa kushirikiana na mashirika ya  FOWARD NA COMOMIC RELIEF ya uingereza.

mkoa mara nikati ya mikoa ambayo inawasichana wengi waliopata mimba  chini ya umri mdogo  kutokana nachangamoto mbalimbali za kifamilia,nawengine wakichangiwa na tamaa za kimwili na malezi yao.

UMAT  nimrdi ambao umelenga kuwa saidia wasichana walio mazingira hatarishi naambao waliopata mimba chini ya umri mdogo ilikuzitambua fursa za kiuchumi zinazowazunguka ikiwemo kuwapatia  mitaji midogo midogo zitakazo wawezesha kujikwamua kimaisha.

lakini pia mradi huo umelenga kuondo ukatili wa kijinsia kwa wasichana na mimba za utotoni nahata mimba kwani zinawakwamisha kutoyafikia malengo yao ambayo wamejiwekea wao
 
UMATI, kwa kushirikiana na mashirikika ya FORWARD na COMIC RELIEF  kwa madhumuni yakuondoa vikwazo vinavyomkabili mtoto wakike nakumuwezesha kuyafikia malengo yake.

    ''  tunaendasha makongamano yakuondoa ndoa za utotoni nakutokomeza        kabisha  nahata mimba za utotoni tunatoa elimu kwakushirikisha hamalashauri na wadau mbalimbali'' alisema BARNABA RICHARD.

BARNABA RICHARD ambae yeye ni afisa mradi wa UMAT amesema wanakutana na wazazi ,viongozi wadini na kimila,wenye viti wa vijiji kwa  ajili yakuwapatia elimu ilikufaham haki za mtoto wa kike,mambo ya ukeketaji.

amezitaja kata ambazo wameanza  kuwasaidia wasichana hao ambao wamewawezesha huku wakianza nakata tano ikiwemo NYEGINA, ETARO,NYAKANGA, NYAMIMANGO,na KUKIRANGO.


Baadhi ya Wasichana wanaopata mimba chini ya umri mdogo imebainika kuwa wengi wao mimba hizo zinanchagiwa na wazazi wao kutokana nakushindwa kuwapa malezi yanayotakiwa.


Akizungumza na MAKALI BLOG ,Ferista ndilanga mashauri yeye nibinti mwenye umri wamiaka kuminane yeye alipata ujauzito akiwa kidato cha tatu hivyo kukatisha masomo yake nasasa Kutokana na elimu aliyoipata kutoka kwa UMATI itamuwezesha kuendesha maisha yake nakuwawezesha wengine kupata elimu aliyoipata yeye kutoka kwa umati.


Aidha  baadhi ya wasicha ambao nao wamepata mimba chini ya umri wa miaka kumi nanane wamewataka mabinti ambao hawajapata ujauzito kuweza kujilinda nakuziepuka mimba za utotoni ndoa za utotoni kwani zinakatisha malengo ambayo ulikuwa umeyapanga.

Nae meneja mradi kanda UMMATI bw nyangwengwe  wango amewataka mabinti hao kwenda kuzitumia vyema fedha ambazo wamepewa kwa ajili yakuendeleza biashara zao ambapo fedha hizo zitawainua kiuchumi.
Powered by Blogger.