Waliohukumiwa adhabu ya Kifo nchini Kenya Wabadilishiwa Hukumu
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametatilisha hukumu ya wafungwa zaidi ya elfu mbili ambao walikuwa wamehukumiwa kifo.
Rais amebadilisha hukumu hiyo na sasa wafungwa hao 2,747 watatumikia hukumu ya maisha jela.
Wahalifu wamekuwa wakihukumiwa kifo Kenya lakini hakuna aliyewahi kuuawa tangu miaka ya 1980.
Watetezi wa haki wamekuwa wakipigania kuondolewa kwa hukumu hiyo.
Baadhi
ya wafungwa hata hivyo wamekuwa wakilalamika kwamba hakuna tofauti ya
hukumu ya kifo na maisha jela kwani mfungwa huwa anaishi jela hadi kifo
chake.
Rais Kenyatta pia amewaachilia huru wafungwa 102 waliokuwa wakitumikia vifungo virefu.
Alhamisi
wiki iliyopita, Rais Kenyatta alikuwa amewaachilia huru wafungwa
takriban 7,000 wa makosa madogo madogo au waliokuwa wanakaribia kumaliza
kutumikia vifungo vyao, na ambao walikuwa wameonyesha dalili za
kubadilisha tabia.