Ushahidi wa kiapo cha mshitakiwa wa kwanza katika kesi ya uchaguzi jimbo la Bunda Mjini waleta utata Mahakamani.

Ushahi wa kiapo  cha Mshitakiwa wa kwanza katika kesi namba moja ya mwaka 2015 ya kupinga matokeo yauchaguzi katika jimbo la Bunda mjini Ester Bulaya, leo umeleta utata wa kisheria kuhusu utoaji wa ushahidi   uliomkwamisha Mbunge wa Jimbo la Bunda mjini  Bulaya kutoa ushahidi wake, katika kesi inayoendelea mjini Musoma mkoani Mara.

Hatua hiyo ilitokana na  malumbano ya kisheria kati ya mawakili wa upande wa waleta maombi na wakili upande wa  utetezi hali iliyosababisha jaji  Noel Chocha anayesikiliza kesi hiyo kuahirisha kesi hiyo hadi kesho mchana.

Utata huo ulitokana na wakili Constantine Mutalemwa wa upande wa waleta maombi kuweka pingamizi katika baadhi ya aya zilizokuwepo kwenye  hati ya kiapo cha shahidi huyo, hatua iliyozua mjadala mkubwa  kati  ya wakili huyo na wakili wa upande wa utetezi Tundu Lissu.

Katika mjadala huo kila wakili alijaribu kutetea hoja yake, huku kila mmoja akijaribu kutoa vifungu vya sheria ,ambavyo vinaonyesha msingi wa  hoja  anayoitoa.

Wakili Constantine Mutalemwa alisema kuwa  aya hizo ambazo aliiomba mahakama ziondolewe, zilikuwa   zinapingana na matakwa  ya sheria  ya kanuni na sheria  za kuongoza  mashauri ya  kesi za madai ya uchaguzi. kwamba ni tofauti na  kesi za mashauri ya kesi nyingine  hivyo shahidi anapaswa kutoa ushadhidi anaoufahamu mwenyewe na sio wa kuelezwa  na shahidi mwingine na kama ameambiwa anatakiwa ajue vyanzo vya taarifa hiyo.

Mutalemwa alisema kati  ya aya 11 zilizosomwa na mjibu maombi wa kwanza katika kiapo chake  zinazotakiwa kubaki katika kiapo hicho ni aya 4 ambazo ndizo zilizoonekana kuwa hazina utata wowote na ambazo wanakubaliana nazo kabisa bila kuwa na shaka.

Mutalemwa alizitaja aya ambazo  zilitakiwa  kuondolewa  kwenye kiapo hicho cha shahidi wa kwanza kuwa ni pamoja na   aya ya 2,3,4,5,6,7,8,ambazo zilikuwa zinaibua hoja mpya ambazo zilikuwa hazikutajwa kwenye majibu yao wakati wakijibu maombi katika hatua za awali.

Kufuatia mjadala huo wa kisheria, jaji  anayesikiliza kesi hiyo  Noel Chocha ameamua kuahirisha kesi hiyo ili kwenda kupitia  hoja hizo kabla ya kufanya maamuzi huku akisema kuwa suala hilo lilihitaji muda mrefu ili aweze kupitia sheria na kufanya maamuzi sahihi.


Kutokana na hali hiyo Jaji Chocha aliamua kuahirisha kesi hiyo hadi kesho (leo) saa saba ambapo ataleta maammuzi ya kutathmini  ubora  namna ya uamuzio kuhusu mabishano ya kisheria juu ya kiapo hicho na aya znazotakiwa kuondolewa ama kutoondolewa.

Awali mshitakiwa wa kwanza katika kesi hiyo Ester Bulaya alishindwa kusoma kiapo cha ushahidi kwa madai kutokana na sheria za lugha za mahakama .

Aidha alimuomba Wakili wa  alichukua muda wa saa tano kutoa utetezi wake huku akidai uchaguzi huo hauukuwa huru na haki kutokana na kukgubikwa kwa wimbi la ongezeli Mshitakiwa namba moja katika kesi hiyo Ester Bulaya  alishindwa  kusoma kiapo kutokana na  sheria za lugha za mahakama  zinatumika japo  kuwa alimueleza jaji ameiandaa yeye baada Jaji kumuuliza ataweza kusoma na kumuomba wakili wa wajibu maombi Tundu Lisu kumosomea.

Lisu akisoma Kiapo hicho kwa niaba yake alidai kuwa alichaguliwa  kihalali  kwa idadi ya kura 28,568 dhidi ya 19,126 alizopata mgombea  wa CCM na kwamba idadi ya vituo  vilikuwa 190 na si 199 na hakuna kampeni haramu zilizofanyika siku ya kupiga kura na kuhusu fomu ya gharama za uchaguzi alizijaza  Agosti  20 mwaka 2015 .

Aliosema alipata barua ya mwaliko kutoka kwa Kaimu katibu wa  wilaya ya Bunda CHADEMA  Yohana kahunya   ya kiapo chake  iliyotoka kwa msimamizi  wa uchaguzi  iliyokuwa imetumwa kwa wagombea wote watano ikionyesha taerehe, muda na mahali pa kuhesabia kura na kutangazia matokeo.
Powered by Blogger.