MWALIMU AUAWA KISHA KUNYOFOLEWA MKONO HUKO DODOMA
Mwalimu Israel Mlowasa (40) wa Shule ya Sekondari Nkuhungu katika Manispaa ya Dodoma, amekutwa ameuawa nyumbani kwake na kiganja chake cha mkono wa kulia kukatwa na kuondoka na wauaji hao.
Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi inasema kwamba mauaji hayo yamefanyika juzi maeneo ya Chang’ombe Extension katika Manispaa ya Dodoma.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Nkuhungu, Fidelis Kaishozi alisema mwalimu huyo alipotea tangu Oktoba 2, mwaka huu na taarifa kutolewa Polisi.
Imeelezwa kuwa maiti ya mwalimu huyo ilikutwa katika pagala la nyumba eneo la Nkuhungu.
Hakuna mtu aliyekamatwa kuhusu mauaji hayo, msako mkali unaendelea ili kubaini wahusika na mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Rufaa Dodoma kwa uchunguzi zaidi wa madaktari.