Msafara wa JPM wakumbana na foleni, mwenyewe ataka kutembea kwa miguu
Katika
hali ambayo sio ya kawaida kwa kiongozi kama rais wa nchi, Rais John
Magufuli ambaye yupo nchini Kenya kwa ziara ya kiserikali ya siku mbili
amekutana na foleni wakati akielekea katika eneo ambalo alizikwa Rais wa
kwanza wa Kenya, Jomo Kenyatta.
Kwa
mujibu wa shuhuda wa tukio hilo, aliuambia mtandao wa Star wa Kenya
kuwa Rais Magufuli alikutana na foleni hiyo wakati akitokea katika
hoteli ya Intercontinental na kuelekea eneo la alilozikwa Jomo Kenyatta
na baada ya kuona kuna foleni kubwa alitaka kutembea ili aweze kufika
eneo ambalo anataka kwenda kuliona.
Aidha
baada ya kutoka eneo hilo alikuta tayari maafisa wa usalama wameshaweka
magari mengine pembeni ya barabara ya Uhuru na hivyo aliweza kupita kwa
urahisi kuelekea ikulu kukutana na mwenyeji wake, Rais Uhuru Kenyatta.
Baada ya kuwasili ikulu JPM alionana na Rais Kenyatta na kufanya mazungumzo kisha kulihutubia taifa la Kenya kuhusu mahusiano ya Kenya na Tanzania na mipango ambayo wameiweka baada ya kufanya mazungumzo.