Makamba asikitishwa na upungufu wa maji katika Ziwa Rukwa, atoa maagizo kwa wakurugenzi
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.January
Makamba ameendelea na ziara ya kikazi katika Mkoa wa Rukwa. Katika ziara
yake Waziri Makamba ameshuhudia uharibifumkubwa wa mazingira hususan
pembezoni mwa ziwa Rukwa.
Waziri Makamba amewaambiwa wakazi
wa Kijiji cha Nankanga kwambamwaka 2000 kina cha maji katika ziwa Rukwa
kilikuwa ni mita sita, na kwa mwaka 2016 chanzo hicho kimepungua hadi
kufikia mita tatu.
“Tafitivzinaonyesha kuwa kupungua
kwa kina hicho pamoja na mambo mengine kunasababishwa na kilimo cha
milimani na kandokando ya ziwa, na ulishajiwa mifugo katika Vyanzo vya
maji,” Makamba alibainisha.
Katika ziara yake baada ya
kushuhudia uharibifu mkubwa kiasi hicho, Waziri Makamba ameazimia
kulitangaza eneo la Ziwa Rukwa kama eneo mahsusi kwa mazingira na kanuni
za matumizi ya maeneo hayo zitaandaliwa ilikunusuru Ziwa Rukwa.
Pia, wakurugenzi wote wa
Halmashauri za Mkoa wa Rukwa wameagizwa kutenga pesa zitokanazo na tozo
mbalimbali ili waweze kugharamia uwekaji wa alama maalumu ‘beacons’ ili
kuainisha eneo tengefu na kuagiza kuwazoezi hili lifanyike haraka.
Aidha, Mhe. Makamba amesisitiza
juu ya upandaji wa miti na ameonyesha masikitiko yake kwa Mkoa wa Rukwa
kuwa na upungufu wa miti ya asili na ileya kupanda kwa kiwango kikubwa.
“nimetembea zaidi ya kilomita 200 sijaona miti iliyopandwa,” Makamba
aliongezea.
Wakazi wa Mkoa wa Rukwa
wamefahamishwa na kusisitizwa kuwa kuanzia mwakani itakuwa lazima kwa
wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kuripoti na miti na kutakiwa
kuitunza mpaka pale watakapomaliza shule. Waziri Makamba ameahidi kuleta
wataalamu na kutoa orodha ya miche inayostawi katika kila kijiiji ili
kurahisisha uoteshaji wa miti.
Katika hatua nyingine, Waziri
Makamba amekutana na viongozi mbalimbaliza dini na wazee wa Mkoa wa
Rukwa na kuwataka kuunda Kamati ya Amani,na kuahidi kugharimia Mkutano
wa kwanza wa kuundwa kwa baraza hilo nakusisitiza agenda ya mazingira
iwepo.
Mkoani Rukwa Waziri Makamba
ametembelea mwalo wa ziwa Rukwa na kuzungumza na wananchi wa maeneo hayo
na Mkutano wa Hadhara katika
Kijiji cha Nankanga ambapo wakazi
wa maeneo hayo wamempongeza kwakua toka kijiji hicho kianzishwe mwaka
1974, Waziri Makamba ndio amekuwa mgeni wa kwanza Kitaifa kuwatembelea.