kocha-wa-yanga-hans-van-der-pluijm-akiwa-na-benchi-lake-la-ufundi_1vssjdt7646et1r82ihmt2znkp

Kocha Hansa Van Pluijm aliejiunga na Yanga SC msimu wa 2013-14 na kuifikisha timu hiyo nafasi ya pili kuu Tanzania bara nyuma ya Azam FC walionyakua ubingwa huo kwa mara ya kwanza, ameifanyia makubwa timu ya Yanga lakini msimu wa mafanikio kwake ukiwa msimu wa 2015-16 baada ya kurudi tena kupokea timu kwa mbrazili Macio Maximo.

Msimu wa ligi kuu 2015-16 Hans Van Pluijm aliiwezesha timu hiyo kutwaa kombe la ligi kuu ikiwa imecheza michezo 30 na kupoteza mchezo mmoja tu dhidi ya Coastal Union mjini Tanga na kwenda sare mechi 7.
Rekodi ya kupoteza mechi 1 tu katika mechi 30 huku mchezaji wake Amisi Tambwe akiibuka mfungaji bora wa ligi kuu kwa goli 21 hii inaonesha uwezo wa kocha huyo kuisuka vyema timu yake katika safu ya ulinzi na ushambuliaji.
Msimu huo huo wa 2016 Hans Van aliiwezesha Yanga kutwaa kombe la FA baada ya kushinda mechi zote saba toka mechi za mtoana, robo fainali, nusu fainali na fainali dhidi ya Azam FC.
Hii ni jumla ya mechi 29 kati ya mechi 37 katika kombe la ligi kuu na na FA Pluijm aliiwezsha Yanga kushinda kwa msimu wa 2015-16.
Hatua ya awali kombe la klabu bingwa barani Afrika Pluijm aliiwezsha Yanga kushinda mechi 3. Alishinda dhidi ya Cercle de Joachim nyumbani na ugenini ikiwa ni jumla ya mechi 2 pia akishinda mechi moja dhidi ya APR na kutoka sare mechi ya marudiano jijini Dar.
Hatua ya pili klabu bingwa alikwenda sare mara moja dhidi ya Al Ahly jijini Dar ( 1-1 ) na kufungwa 2-1 jijini Alexandria Misri. Hii ni wastani wa kushinda mechi 3 klabu bingwa , sare 2 na kufungwa mechi 1.
Kombe la Shirikisho Hans Van Pluim alishinda mechi 2 tu moja ikiwa hatua ya raundi ya pili dhidi ya Esperanca Sagrada 2-0 jijini Dar na kufungwa 1-0 nchini Angola. Hatua ya nane bora alishinda mechi 1 tu dhidi ya MO Bejaia jijini Dar na kupoteza mechi 5.
Msimu mpya wa ligi kuu Tanzania bara mechi ya Ngao ya Jamii alipoteza kwa matuta dhidi ya Azam FC lakini ameweza kuiongoza Yanga kushinda mechi 6 sare mechi 3 na kufungwa mechi 1 ikiwa nafasi ya 2 katika ligi na alama 21.
REKODI MUHIMU
Anashikiria rekodi ya kocha bora wa msimu wa 2015-16
REKODI KITIMU
– Mabingwa ligi kuu msimu wa 2015-16
-Mabingwa kombe la FA msimu wa 2015-16
– Kufika raundi ya pili klabu bingwa Afrika 2016
– Kufika hatua ya nane bora kombe la shirikisho2016
Wachezaji
Katika msimu wa 2015-16 amemuwezesha beki wake wa kulia Juma Abduli kuibuka mchezaji bora wa mwaka katika ligi kuu Tanzania bara.
Thabani Kamusoko kutokana na mbinu zake za ufundishaji na kusimamia nidhamu katika timu mchezaji huyo toka nchini Zimbabwe aliibuka mchezaji bora wa kigeni na kunyakua tuzo ya Vodacom kama wadhamini wa ligi.
Amisi Tambwe chini ya ukufunzi wake amefanikiwa kuibuka mfungaji bora baada ya Hans Van Pluijm kutengeneza kombinesheni nzuri ya ushambuliaji katika mshambuliaji huyo na mzimbabwe Donald Ngoma.
Tayari uongozi wa Yanga umeshamleta Kocha mpya Mzambia
 Hans Van Pluijm Hans Van Pluijm