Chama Cha Walimu Tanzania kimeipongeza serikali kwa kuanzisha zoezi la utambuzi wa wafanyakazi hewa

 c

Chama Cha Walimu Tanzania CWT kimeipongeza serikali kwa kuanzisha zoezi la utambuzi wa wafanyakazi hewa huku chama hicho  kikiiomba serikali kuhakikisha zoezi hilo linaende sambamba na ufumbuzi wa matatizo yao ikiwemo upandishwaji wa madaraja kwa wakati,mishahara midogo,malimbikizo ya madeni yao  na uhaba wa nyumba za kuishi.

Kauli hiyo inatolewa mkoani Arusha  na rais wa chama cha walimu Tanzania Gratian Mukoba katika tukio lililo wakutanisha   kwa pamoja walimu wa wilaya  ya Arumeru na walimu  wengine kutoka mikoa ya kanda ya kaskazini,ambapo Mukoba ameendelea kuiomba serikali kutimiza baaadhi ya ahadi zake dhidi ya madai ya walimu ambayo amedai kwa kiasi fulani yamekuwa ya muda murefu.
Joyce Kijazi ni Katibu wa chama cha walimu wilaya ya Arumeru, anasema  iko haja ya kuboresha idara ya ukaguzi wa shule na kuongeza umakini kwa baadhi ya watendaji wanao shughulikia masuala ya walimu katika ngazi za wizara na halmashauri.
Kwa mujibu wa Taarifa kutoka CWT wilaya ya Arumeru mpaka kufika september 2016  walimu wanaidai serikali zaidi ya shilingi Bilioni moja nukta nne ikiwa ni malimbikizo toka mwaka 2009 ambayo tayari yamehakikiwa.
Powered by Blogger.