Baada ya jamaa Arusha kutoa siku 30 kwa wezi, ajiandaa kuvunja chungu
Tumezoea
mtu akituhumiwa kwa wizi anapelekwa mahakamani lakini hii imekuwa
tofauti kwenye mila za kabila la Wameru na wamasai Arusha Tanzania,
ambapo mtu akikutwa na tuhuma kama za wizi kuna kitu kinaitwa kuvunja
chungu.
Utaratibu
wa kuvunja chungu umezoeleka sana kwa makabila yakimeru na kimasai na
huvunjwa baada ya makubaliano na huwa kinamhusu ambaye amehusika kama
kwa tukio la wizi.
Unaambiwa
zamani chungu kilikuwa kikivunjwa, ukoo uliovunjiwa chungu wataanza kufa
mashangazi mpaka ukoo unaisha, sasa hivi kikivunjwa analengwa mhusika
au kama wawili walipanga kufanya tukio la wizi.
Sasa
Katika kata ya Makuyuni wilaya ya Monduli Arusha Mohamedi Olodi amepanga
kuvunja chungu kwa waliomvunjia duka lake na kuiba bidhaa na fedha
zenye thamani ya zaidi ya Milioni 2.