MKUU WA MKOA WA MARA AZITAKA HALMASHAURI KUSIMAMIA FEDHA ZA RUZUKU ZINAZOTELEWA NA AGPAHI



Menejea wa AGPAHI kanda ya Ziwa Dr.Nkingwa Mabelele akiwasilisha taarifa katika kikao cha RCC katika ukumbi wa uwekezaji.
Mganga Mkuuu wamkoa wa Mara Dr. DR.Fransinci Mwanisi akiwasilisha Taarifa katika kikao cha Ushauri( RCC) mpango wa utekelezaji wa utaoji huduma za afya kwa mwaka 2017/2018. 

Kushoto aliyevalia miwani ni Meneja wa kanda ya Ziwa kutoka AGPAHI Dr. Nkingwa Mabelele akifatilia wakati wa uwasilishwaji wa taarifa katika kikao cha ushauri ya mkoa wa Mara( RCC).

Baadhi ya wajumbe waliohudhulia katika kikao hicho.
Wajumbe kikao cha ushauri ya mkoa (RCC) wakifatilia Mkutano huo.

Sehemu ya viongozi wa PCCI wakifatilia taarifa za Mkoa wa Mara

Viongozi wa mkoa wakiwemo Wakuu wawilaya na Wabunge wakiwasikiliza uwasilishwaji wa taariifa ya mpango wa utekelezaji wa miradi ya maji kwenye vijiji vilivyopo kandokando ya ziwa Victoria.

Na Makaliblog.mara
Mkuu wa mkoa wa Mara Mheshimiwa, Adam Malima amesema  atashirikiana vyema na shirika la AGPAHI kutika Shughuli za mapambano ya Virusi vya Ukimwi pamoja na shughuli za maendeleo ambazo zinatekelezwa  katika Mkoani wa Mara.

Aliyasema hayo katika kikao cha kawaida cha kamati ya ushauri ya mkoa wa Mara,( RCC) kilichofanyika katika Ukumbi wa uwekezaji mkoani Mara baada ya meneja wa kanda ya Ziwa kutoka AGPAHI kuwasilisha Taarifa ya utekelezaji wa shughuli na Miradi inayotekelezwa na Shirika hilo.

Malima alisema, upo utayari wa Wakurugenzi wa Wilaya zote za Mkoa wa Mara kuhakikisha wanatoa ushirikiano wa matumizi ya Ruzuku za ukarabati wa Zahanati zinazotolewa na shirika la Agpahi nakuzisimamia ipasavyo fedha hizo kwa nguvu zao zote.

" Simamieni fedha hizi mnaona sisi hapa tunashikana mashati ilikupata bilioni 20 kwa ajili yakukamilisha ukarabati wa hospital ya mwalimu nyerere lakini hawa wanatoa fedha kwa mkupuo, nani pesa nyingi kwahiyo nawagiza mhakikishe mnazisimamia namuwe wepesi, watukutuma taarifa zinazotakiwa kwa hawa Agpahi"alisema malima.

Shirika la Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative (AGPAHI) linajihusisha na mapambano dhidi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi na katika kutekeleza Miradi yake ambapo shirika la Agpahi,linatekeleza Miradi yake katika mikoa saba Nchini Tanzania ikiwemo Geita, Mara,Manyara,Mwanza,Shinyanga,Simiyu na Tanga. Mradi ambao unatekelezwa na shirika hilo katika mkoa wa Mara ni mradi Boresha ambao sasa umeonekana kuwa na manufaa katika maeneo yote unakotekelezwa mradi huo.

Awali Dr. Nkingwa alisema mradi wa Boresha ambao umeanza na mwaka 2016  utaisha mnamo mwaka 2021, alisema fedha za  Ruzuku zinazotolewa zinasaidia  kuratibu shughuli mbalimbali za Ukimwi ili kuboresha utoaji huduma Bora za Afya, pia zilitumika kusaidia Halmashauri kufanya usimamizi na ufatiliaji katika maeneo husika, Pia Ruzuku hizo zimesaidia Vituo vya afya kununua vifaa vya tiba ikiwemo kifaa cha kuangalia wingi wa Virusi vya Ukimwi(VVU).

Kwa kipindi cha Oktoba 2016 hadi Septemba 2017 Shirika la AGPAHI limefanikiwa kuwapima zaidi ya watu 199,889 na kati ya hao watu 7325 walikutwa na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi(VVU).

Akichangia katika Taarifa hiyo,Mganga mkuu wa Mkoa wa Mara, Dkt.Fransinci Mwanisi alisema, kwa ushirikiano unaotolewa na shirika hilo ni vyema ukaungwa mkono kwani wamekuwa wakisaidiana sehemu kubwa za huduma za afya katika vituo vya afya mkoani mara.

Aidha mkuu wa wilaya ya Musoma Dr.Vicent Naano, ameliomba shirika la Agpahi kuzishirikisha Halmashauri wakati wa upangaji wa Ruzuku za miradi ambayo inapangwa kutekelezwa kwani itasaidia kuondoa changamoto kubwa katika vituo hivyo.

kikao cha kawaida cha kamati ya ushauri ya mkoa( RCC) nikikao  ambacho kinawakutanisha  wajumbe kujadili Taarifa za utekelezaji wa miradi mbalimbali ambapo kinakuwa nikikao cha kawaida cha kamati ya ushauri ya mkoa ambacho kinakaa mara mbili kwa mwaka katika mkoa wa mara.
Powered by Blogger.