HARUSI ISIYO NA GHARAMA YAZUA GUMZO..WAMETUMIA SHILINGI ELFU 2 TU..SHUHUDIA
Wanandoa wawili ambao taarifa yao ya
harusi isiyo na gharama imezua gumzo na imevutia watu wengi katika
mitandao ya kijamii na sasa watagharamiwa honeymoon (fungate) ya harusi
hiyo.
Wilson mwenye umri wa miaka 26 na Ann
Wambui mwenye umri wa miaka 24 alitumia shilingi za Kenya 100 sawa na
shilingi 2,147 ya Tanzania,kununua pete mbili mbali na kuvaa tisheti za
sherehe hiyo.
Hawakuwa na sherehe yoyote baadaye.
''Tulienda nyumbani, tukapika ugali na
sukuma wiki tukala na kulala,hapakuwa na kitu chochote maalum ambapo
tungefanya kama fungate yetu'', kulingana na eDaily News.
Kiongozi wa dini ambaye alihalalisha
ndoa hiyo alisambaza habari yao katika mtandao wa facebook kabla ya
kuchukuliwa na vyombo vya habari.
Mwakilishi wa kampuni ya Bonfire Adventure alikutana na wanandoa hao.
Wilson na Ann Wambui wakifunga ndoa
Wilson na Ann Wambui