Askari wa SUMA JKT Watiwa mbaroni kwa kuua Wafugaji Wanne na kujeruhi Watano
Jeshi
la polisi mkoa wa Arusha, linawashikilia Askari wanne wa SUMA JKT kwa
tuhuma za kuhusika kuwaua wafugaji wanne kwa kuwapiga risasi na
kuwajeruhi wengine watano kwenye vurugu zilizotokea eneo la Oldobnyo
Sambu wilayani Arumeru.
Kamanda
wa jeshi la polisi mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo, alisema chanzo cha
mauaji hayo ni wafugaji wa kimaasai kuwavamia askari hao ambao walikuwa
wamekamata ng’ombe ambao waliingizwa ndani ya msitu wa hifadhi ambao ni
wa serikali, kwa ajili ya malisho, kutokana na ukosefu wa malisho.
Kamanda,
Mkumbo,amesema Askari hao ambao wanalinda msitu huo maarufu , shamba la
miti la Meru USA Plant ,ambalo ni la serikali, walianza oparesheni zao
majira ya saa 2.30 asubuhi za kuondoa mifugo iliyoingizwa ndani ya msitu
huo.
Askari
hao wa SUMA JKT, awali walikamata ng’ombe 45 , mbuzi na kondoo 65 na
kuwapeleka kwenye zizi maalumu lililopo kituo cha polisi Oldonyo Sambu.
Askari
hao waliendelea na oparesheni hiyo na ilipofika majira ya saa 8 mchana
walipata taarifa ya kuwepo kwa kundi jingine katika msitu huo na
kufanikiwa kukamata ng’ombe 80, mbuzi na kondoo 70 kwa lengo la
kuwapeleka kwenye zizi hilo la serikali.
Amesema
wakati wanawaswaga mifugo hao ndipo kundi la wananchi wakiwa na silaha
za jadi walipojitokeza mbele yao wakitaka kuwakomboa mifugo hao kwa
nguvu.
Hatua hiyo iliwalazimu askari nao kuanza kuwafyatulia risasi na kusababisha vifo vya vijana wanne na watano kujeruhiwa.
Amewataja
wananchi waliouawa kuwa ni Mbayan Melau (27), Julius Kilusu (45),
Lalasehe Meibuko (25), na Seuri Malita (32) na hakuna askari
aliyejeruhiwa.
Diwani
wa kata ya Oldonyo Sambu, Raymond Lairumbe amesema hatazika miili hiyo,
mpaka viongozi wa serikali watakapofika eneo hilo kuzungumza nao na
huku majeruhi wanne waliolazwa hospitali ya Mount Meru Arusha, wakiomba
msaada wa kutolewa risasi katika miili yao.