MWANAFUNZI WA DARA LA 5 AJINYONGA
Mwanafunzi wa darasa la tano katika Shule ya Msingi Kizota mjini Dodoma, Yasin Abdallah (13) amekutwa amejinyonga bafuni nyumbani kwao baada ya kuchukizwa kufanya vibaya kwenye masomo yake.
Kaimu
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Ernest Kimoli alisema tukio hilo
lilitokea Desemba 2 eneo la Kizota Relini Manispaa ya Dodoma.
Kimoli alisema baba mzazi wa mtoto huyo, Hassan Juma (53) aligundua kujinyonga kwa mwanaye saa 6:00 mchana.
“Sababu ya kujinyonga ni kuchukizwa na matokeo ya mitihani yake,” alisema.
Diwani wa Kizota, Jamary Ngalya alisema mtoto huyo ambaye alizikwa juzi jioni, alianza kwa kuwaeleza wanafunzi wenzake Ijumaa kuwa atajinyonga.
Diwani wa Kizota, Jamary Ngalya alisema mtoto huyo ambaye alizikwa juzi jioni, alianza kwa kuwaeleza wanafunzi wenzake Ijumaa kuwa atajinyonga.
Alisema
baada ya kutamka maneno hayo, wenzake walimwambia wanakwenda kumweleza
mwalimu. Hata hivyo, baada ya kuwasikia wenzake aliwaambia kuwa anatania
hawezi kufanya hivyo.
“Katika matokeo ya kumaliza darasa la nne alikuwa wa 129 kati ya 132, inawezekana huko alikuwa anafanya vizuri,” alisema