WANANCHI WAMUOMBA MKUU WA MKOA WA MARA KUINGILIA MGOGORO WA KATA YA GWIKO ,RUNYERERE NA MABUTE

Wananchi wa kijiji cha Turugeti Kata Ya Bumera Wilayani Tarime mkoani Mara wameomba kutatuliwa  Mgogoro wa ardhi uliokuwepo baina ya kata ya Nyandoto na kata ya Bumera  ili kuweza kutoa maamuzi ya mwisho kwani wamedai  kuwa maamuzi yaliyotolewa na mkuu wa wilaya ya Tarime Glorious Luoga hawakubaliani nayo nakuomba itumike ramani ya mwaka 1988 katika  kubaini mipaka hiyo.



 wananchi hao wamesema kuwa hawakutendewa haki baada ya kunyang'anywa vitongoji vitatu ambavyo ni Gwiko,Runyerere, na Mabute na kupelekwa Gamasara huku wakidai kuwa ramani iliyotumika kukata vitongoji hivyo siyo sahihi bali watumie ramani ya mwaka 1988.




Baada ya kero hiyo kipindi hiki kimemtafuta mkuu wa wilaya tarime GLORIUS LUOGA ilikujibu tuhuma hizo ambapo amesema kuwa  kuwa Mgogoro ulikwisha  mwaka 2006  na mku wa wilaya aliyekuwepo kipindi hicho Stanley Korimba bali mgogoro unaibuka kwa sasa unasababishwa na mwenyekiti wa kijiji cha Turugeti aliyechaguliwa mwaka 2008

Ambapo amesema mwenyekiti huyo ambae anaedekeza mgogoro huo amekuwa akifanya kwa manufaa ya ukoo wake akilima ndugu yake katika mpaka basi mpaka huo nakuuchukua kuwa wakwake luoga ametoa ufafanuzi huyu hapa.



Aidha  mkuu wa wilaya amesema kuwa hawatamvumilia kiongozi yoyote anaendekeza migogoro ya mipaka ambapo amesema tarime ndio pekee wanaolalamikia mipaka ambapo kila mtu anafahamu mpaka wake.
Powered by Blogger.