Rais Dkt. Magufuli afungua barabara ya Nairobi Southern Bypass Nchini Kenya
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa
Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta leo tarehe 01 Novemba, 2016
wamezindua barabara ya Southern By-pass iliyojengwa kwa lengo la
kupunguza msongamano wa magari katika Jiji la Nairobi nchini Kenya.
Sherehe
ya uzinduzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 28 na
inayounganisha maeneo mbalimbali ya Jiji la Nairobi imefanyika katika
eneo la Karen nje kidogo ya Jiji la Nairobi.
Akizungumza
katika sherehe hiyo Rais Magufuli amempongeza Rais Kenyatta na Serikali
yake kwa kujenga barabara hiyo ambayo sio tu itawasaidia wananchi wa
Kenya bali pia itawasaidia wananchi wa Afrika Mashariki wanaotumia
barabara zinazopitia Nairobi.
Rais
Magufuli pia ameishukuru Serikali ya China kupitia benki yake ya Exim
ambayo imetoa mkopo wa kujenga barabara hiyo, kwa kuendelea kuziamini
nchi za Afrika Mashariki na kuzikopesha mikopo inayosaidia utekelezaji
wa miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara.
“Wananchi
wanahitaji maendeleo na haya ndio maendeleo, barabara hii itasaidia
kuinua uchumi na itasaidia masuala ya kijamii” amesema Rais Magufuli.
Dkt.
Magufuli amesema viongozi wa Afrika Mashariki wameamua kufanya kazi ya
kuharakisha maendeleo na kuinua maisha ya wananchi, na kwamba ili
kufanikisha hilo wamedhamiria kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo
ujenzi wa barabara zinazounganisha nchi wanachama na kujenga vituo vya
pamoja vya utoaji wa huduma za mpakani (One Stop Border Post).
Kwa
upande wake Rais Kenyatta amesema kujengwa kwa barabara hiyo kumesaidia
kupunguza msongamano wa magari katika Jiji la Nairobi na pia
kutaboresha shughuli za maendeleo ya wananchi.
Mhe.
Kenyatta amemshukuru Rais Magufuli kwa kuungana nae kuzindua barabara
hiyo na amesema Kenya itaongeza juhudi katika utekelezaji mradi wa
ujenzi wa barabara zinazounganisha Kenya na Tanzania zikiwemo barabara
ya Malindi kupitia Saadani hadi Bagamoyo nchini Tanzania na barabara ya
Voi – Taveta- Holili-Arusha.Sherehe za uzinduzi wa barabara ya Southern
By-pass zimehudhuriwa na Naibu Rais wa Kenya Mhe. William Ruto.
Kabla
ya kuzindua barabara hiyo Rais Magufuli ametembelea kiwanda kidogo cha
kusindika maziwa cha Eldoville kilichopo katika eneo la Karen ambacho
kinamilikiwa na familia ya mkulima Bw. James Karuga.
Familia
hiyo ilianzisha kiwanda cha kusindika maziwa mwaka 1985 kwa uzalishaji
wa chini ya lita 1,000 kwa siku na hivi sasa imefikia uzalishaji wa lita
5,000 kwa siku na inatarajia kuongeza uzalishaji hadi lita 70,000
katika mwaka mmoja ujao baada ya kuongeza kiwanda cha pili.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Nairobi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na
mwenyeji wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, wakiweka jiwa la msingi kuashiria ufunguzi wa
barabara ya kupunguza msongamano ya Nairobi Southern Bypass nchini
Kenya.
mwenyeji wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, wakiweka jiwa la msingi kuashiria ufunguzi wa
barabara ya kupunguza msongamano ya Nairobi Southern Bypass nchini
Kenya.